Wakati watahiniwa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) likizua matokeo ya watahiniwa 31, 518 kutokana na kutolipa ada ya mtihani huo, wengine 282 wamefutiwa matokeo yao kutokana na kubainika kufanya udanganyifu.
Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde alisema kati ya waliofutiwa matokeo, wamo 10 waliobainika kuandika matusi.
Alisema watahiniwa 61 walikutwa na karatasi za
kutazamia, 171 majibu yao walikuwa na mfanano usio wa kawaida, wanne
walikutwa na simu, tisa walifanyiwa mitihani na watu wengine, 13
karatasi zao za majibu zilikuwa na hati (miandiko) zaidi ya moja na 14
walikamatwa wakidhamiria kuiba mitihani.
Kati ya waliofutiwa 242 ni wa shule, 19 wa
kujitegemea na 11 wa mtihani wa Maarifa (QT). Alisema idadi ya
waliofutiwa matokeo imeshuka ikilinganishwa na 2012 ambapo waliofutiwa
mitihani walikuwa 789.
Ufaulu kwa masomo
Dk Msonde alisema ufaulu katika masomo umepanda kwa asilimia 0.61 na 16.72 ikilinganishwa na mwaka 2012.
“Watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili,
ambapo asilimia 67.77 ya watahiniwa waliofanya somo hilo wamefaulu. Somo
walilofaulu kwa kiwango cha chini ni Hisabati ambapo asilimia 17.78 ya
watahiniwa ndio waliofaulu somo hilo,” alisema Dk Msonde.
Kumi zilizoshika mkia
Kwa upande wa shule 10 za mwisho kwenye kundi la
shule zenye watahiniwa zaidi ya 40, shule ya kwanza ni Kisima ya Pwani,
Kitongoni ya Kigoma na Tongoni ya Tanga.
Nyingine ni Njechele ya Dar es Salaam, Lumemo ya
Morogoro, Mvuti ya Dar es Salaam, Tambani ya Pwani, Nasibugani ya Pwani,
Ungulu ya Morogoro na Kitonga ya Dar es Salaam.
Shule za mwisho kwenye kundi lenye watahiniwa
chini ya 40 ni Singisa ya Morogoro, Hurui ya Dodoma, Barabarani ya
Ruvuma, Nandanga ya Lindi na Vihokolo ya Mtwara.
Nyingine ni Chongoleani ya Tanga, Likawage ya Lindi, Ngwandi ya Dodoma, Rungwa ya Singida na Uchindile ya Morogoro.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment