Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 19 February 2014

NCCR YATOLEWA NJE MCHAKATO WA UBUNGE KALENGA

Na Oliver Motto, Iringa

WAKATI haraka za kampeni zikiwa tayari zimeanza, Chama cha NCCR Mageuzi kimeshindwa kukidhi vigezo vya kushiriki mchakato wa kugombea kiti cha Ubunge jimbo la Kalenga mkoani Iringa, ambalo nafasi yake iliachwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk William Mgimwa na  Waziri wa fedha Tanzania kufariki dunia January 1, mwaka huu nchini Afrika Kusini wakati akipatiwa matibabu.
Akizungumzia hatua ya mchakato wa uchukuaji wa fomu za ushiriki huo wa kuwania kiti cha Ubunge, msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga Pudensiana Kisaka amesema jumla ya vyama vilivyochukua fomu vilikuwa vine, lakini vilivyofanikiwa kurejesha ni vyama vitatu pekee.
Akitaja vyama vilivyorejesha fomu hizo Kisaka amesema ni CHADEMA, CCM pamoja na Chama cha CHAUSTA, huku NCCR Mageuzi ikishindwa kukidhi vigezo vya sheria ya uchaguzi.
Aidha Kisaka amesema vyama hivyi vyote vitatu vimerudisha fomu siku ya mwisho huku CCM kikiwa chama cha kwanza kurudisha fomu kikifuatiwa na CHADEMA na kisha CHAUSTA.
Amesema "Chama cha NCCR kimechelewa kurudisha fomu na licha ya hivyo bado baadhi ya masharti ya sheria za uchaguzi kilikuwa bado hakijakidhi, kwa hiyo hawatakuwepo kwenye orodha ya vyama ya kwenye ushiriki wa kugombea kiti cha Ubunge jimbo la kalenga na CHAUSTA wao wamefanikiwa kukidhi vigezo, kwa hiyo vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo mdogo ni CHADEMA, CCM na CHAUSTA", alisema Pudensiana Kisaka.
CCM ambayo mgombea wake Godfrey Mgimwa mtoto wa aliyekuwa waziri wa fedha Dr. Mgimwa, huku CHADEMA mgombea wake ni Grace Tendega na CHAUSTA mgombea wake ni Richard Minja.
Grace Tendega aliletwa katika ofisi za msimamizi huyo wa Uchaguzi jimbo la Kalenga akiwa na msafara wa pikipiki 20 na magari 5, huku mgombea wa CCM pamoja na wafuasi na wanachama wake wakitembea kwa miguu hadi katika ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa.
Wakizungumzia kampeni zao wamesema wanataraji ziwe na amani na utulivu, tofauti kabisa na ilivyozoeleka hapo awali kuwa katika kampeni kuna vurugu.
"Lengo la kampeni ni kumpata mgombea anayekubalika na wanakalinga, basi mimi niwaase wananchi washiriki katika mchakato huo kwa amani na utulivu ili waweze kumpata kiongozi atakayewawakirisha kwa njia ya amani na utulivu," Alisema Tendega.
Naye Mgimwa amesema utulivu na amani ni njia pekee itakayosaidia wananchi kumpata kiongozi atakayewasaidia, katika jimbo hilo la Kalenga.
"Cha msingi ninapenda kuwasihi wananchi wetu kuwa na amani na utulivu na sisi kama wanaKalenga na watanzania ningependa tuendeshe kampeni na uchaguzi kwa njia ya amani na ustaarabu," Alisema Mgimwa.
Naye mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa vijijini Delphina Mtavilalo amefafanua juu ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya hivi karibuni inayowataka wana CCM kuacha unyonge.
Mtavilalo amesema kauli hiyo haina maana ya kuwa wanaCCM hawawezi kutumia silaha kupambana na wapinzani wao, bali watatumia maneno kupambana nao.
"Tulipata Uhuru bila kumwaga damu, tunatoa onyo kwa vijana wetu wakiona kuna mapambano yanayohatarisha maisha yao watoe taarifa kwenye vyombo vya dola, ili jeshi la Polisi ambalo ndilo linamamlaka ya kupambana na waharifu lifanye kazi yake," alisema.
Mchakato wa uchukuaji wa fomu hizo za kugombea jimbo la Kalenga ulianza february 9, 2014 huku  Kampeni za uchaguzi huo mdogo zikiwa zimeanza Februari 19 ambapo zitahimishwa Machi 15, huku tarehe ya uchaguzi ikiwa ni Marchi 16.

No comments:

Post a Comment