Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 15 February 2014

IMAMU AMWAGIWA TINDIKALI

IGP Ernest Mangu

Na Mwandishi Wetu, Arusha

IMAMU wa Sawiyatu Qadiria ambaye ni mkazi wa Tindiga eneo la Unga Ltd, Hassan Bashir (33), amemwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali sehemu ya mabegani iliyosambaa maeneo ya mgongoni na shavu la kushoto.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 3:45 usiku maeneo ya msitiki huo.

Hata hivyo, Kamanda alisema upelelezi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kutumia kopo lililokuwa na kimiminika hicho ambacho kimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kujua uhalisia wake.

Akifafanua zaidi, Kamanda Sabas alisema, uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kwamba muda si mrefu kabla ya tukio hilo, Hassan, alikuwa anatokea maeneo ya kituo kikuu cha mabasi cha Arusha baada ya kuachana na wenzake wawili ambao walikuwa wanajadili kikao cha Maulid.

Alisema muda huo wa saa 3:45 alikuwa maeneo ya karibu na kwake Unga Ltd, ndipo alipomuona mtu amesimama kwenye kiambaza cha msikiti, alimsalimia lakini hakumbuki kama alijibiwa.

Alisema wakati akiendelea kuelekea kwake, alihisi kuna mtu anamfuata na alipogeuka ili ajue ni nani, ghafla mtu huyo alimwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali.

Alisema mara baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alikimbia na kuelekea kusikojulikana.

Alisema baada ya taarifa hiyo polisi waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda katika eneo hilo na kukuta kopo dogo ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na kimiminika kinachosaidikiwa kuwa na tindikali.

No comments:

Post a Comment