KESHO ndiyo kesho! Bonanza la Jogging na Global Breaking News 15778 linachukua nafasi kwa kukutanisha michezo ya jogging, mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, bao la kete, drafti, karate na mingine mingi.
Bonanza hilo la bure litafanyika kwa kuanza na mbio za jogging zitakazoanzia katika Uwanja wa Taifa hadi Uwanja wa Mbagala-Zakhem kutakapofanyika baadhi ya michezo huku mingine ikimalizikia katika Ukumbi wa Dar Live.
Meneja wa Kampuni ya Global Pulishers, Abdallah Mrisho ambao ndiyo watoaji huduma ya breaking news, alisema wataitambulisha huduma hiyo inayowawezesha watumiaji wa mtandao wa Vodacom kupata habari za papo kwa papo katika simu ya mkononi.
Rajabu Mteta (KP) ambaye ni mratibu wa bonanza hilo kwa upande wa jogging, aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, kutakuwa na michezo mingi ikiwemo pool table.
“Tutakuwa na Bashnet (Temeke), Mtoni Pool Club (Temeke), Fuoni (Zanzibar), Mashujaa (Ilala) Topland (Kinondoni), Kurasini Cety (Temeke) Mpo Africa (Temeke) na Texas ya Temeke,” alisema KP na kuongeza:
“Tutakuwa na mashindano ya mpira wa miguu kwa upande wa veteran pamoja na netiboli.”
Mratibu huyo alisema mbali na soka, klabu zaidi ya 200 za mkoa wa Dar es Salaam kwa upande wa mbio za taratibu (jogging) zimethibitisha kushiriki bonanza hilo lenye ushindani wa hali ya juu.
KP alisema mbio za taratibu (jogging) zita----zoongozwa na wenyeji, Kejo Jogging Sports Club, zitaanzia uwanja wa taifa majira ya saa 12 na nusu asubuhi hadi ukumbini Dar Live.
Pamoja na michezo hiyo, bonanza likamilishwa kwa shoo kali ya wasanii wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhani ‘H-Baba’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Stamina na Bendi ya Msondo ndani ya Ukumbi wa Dar Live.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment