Na Mwandishi Wetu, Arusha
IMEELEZWA kuwa endapo kama nchi zenye uwezo wa kifedha zitaweza kusaidia nchi maskini ambazo hazina uwezo wa kifedha kwenye masuala ya majanga ya mabadiliko ya tabia nchi basi tatizo hilo litaweza kupungua kwa kiwango kikubwa sana duniani na hivyo kufanya hata sekta mbalimbali kuwa na uwezo wa kusaidia jamii.
Kwa sasa asilimia kubwa ya nchi ambazo zinakabiliwa na changamoto hiyo ya majanga ya mabadiliko tabia nchi zinashindwa kupiga hatua kwa kuwa hazina uwezo wa kifedha wa kutosha kuwasaidia wananchi wakehayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ya dunia ya sayansi ya mabadiliko tabia ya nchi Bw Richard Muyumbi wakati akiongea na wadau wa masula ya mabadiliko ya tabia ya nchi mapema jana jijini Arusha
Muyumbi alidai kuwa suala la mabadiliko tabia ya nchi linakuwa gumu sana kuweza kumalizika kwa haraka kwa kuwa baadhi ya nchi hazina uwezo wa kutenga fungu kubwa sana la kupambana na majanga hayo ya nchi hali ambayo inaongeza sana kasi ya madhara
Alidai kuwa kama watafanya hivyo ni wazi kuwa dunia ya sasa itapunguza sana madhara ambayo yanatokana na suala hilo ambapo pia hata rasilimali za msingi nazo zitaweza kuwanufaisha walengwa
wakati huo huo alizitaka hata Nchi nyingine nazo kuhakikisha kuwa mbali na kuweza kuweka mikakati mbadala ya kupambana na mabadiliko tabia nchi lakini pia ziweze kuweka mikakti ya kutafuta teknolojia mbadala kwa wananchi
Amedai kuwa kwa kuweka teknolojia kutaweza kupunguza tatizo hilo kwa kiwango kwani kwa sasa asilimia kubwa ya wananchi wakumbana na majanga hayo ya mabadiliko tabia nchi kwa kuwa hawana teknolojia za kutosha .
No comments:
Post a Comment