Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 12 February 2014

WABUNGE WAKUNWA NA HIFADHI YA GOMBE KIGOMA

Baadhi ya watalii wakiwa eneo la hifadhi ya Gombe.
Na Ojuku Abraham
WABUNGE ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, wamekunwa na kitendo cha Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia hifadhi yake ya Gombe mkoani Kigoma, kujenga vyumba vinne vya madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kagongo.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa Abdulkarim Shah alitoa pongezi hizo hivi karibuni kufuatia ziara yao katika hifadhi hizo za taifa zilizo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.
Akizungumza kutoka mkoani Kigoma kwa njia ya mtandao, Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete, alisema Kamati hiyo ilitembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio vingi vya utalii, ambavyo endapo vitasimamiwa na kuendelezwa, vinaweza kuchangia ongezeko la pato la taifa.
Wajumbe hao waliopokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo msitu mnene uliopo ndani ya hifadhi hiyo pamoja na maporomoko ya maji ya Kakombe.
<GPL>

No comments:

Post a Comment