Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 8 February 2014

EPZ ZADAIWA KUSHINDWA KUONGEZA AJIRA NA KUWA MZIGO KWA TAIFA



Mhadhiri mwandamizi wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Godius Kahyarara.



Kanda maalumu za kuzalisha bidhaa za kuuza nje (EPZs) zimetajwa kuwa mzigo kwa taifa baada yakushindwa kuongeza ajira na kuzalisha bidhaa za soko la ughaibuni.

Uchambuzi uliofanywa na Umoja wa Ushirikiano wa Kiuchuhumi wa Maendeleo (OECD) umeeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa maeneo haya yanayopewa upendeleo maalumu mwaka 2002 ni ajira 15,000 pekee zilizopatikana.
OECD katika taarifa yake iliyozinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda,  wiki iliyopita inaeleza kuwa tangu kuundwa kanda hizo zimepewa zaidi ya Dola milioni 710 (karibu sawa na trilioni 1.2)  lakini hazijatimiza malengo yaliyokusudiwa.
Ushirikiano huo wa kiuchumi uliukariri utafiti huru uliofanywa mwaka 2012 na asasi zisizo za kiserikali zikiwamo Policy Forum, zilizokosoa kanda hizo.
Ulibainisha kuwa maeneo ya EPZs hayajawa na mchango wa kukuza uchumi, kuzalisha ajira na kuendeleza viwanda vya ndani.
Ilizitaja EPZs kuwa licha ya kutarajiwa kuwa zitazalisha ajira rasmi za kutosha, zimevurunda na kutoa ajira 15,100 pekee, kwa zaidi ya miaka 12 ya kuwapo kwake.
“Kwa hali hii ni kiasi kidogo ikilinganishwa na misamaha na vivutio vya uwekezaji iliyotolewa. Ilieleza na kuongeza kuwa  ni kama ilitumia Dola  47,000  (Sh milioni 76) kuzalisha kazi moja.
Akitoa maelezo ya dhana ya EPZs mhadhiri mwandamizi wa uchumi wa  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Godius Kahyarara alisema EPZ ni kanda zinazotengenezwa maalumu ili kupunguza vikwazo vinavyotatiza biashara ya nje.
Alisema ili EPZs zifanikiwe serikali inazipa mazingira ya kiupendeleo kwenye kodi, ushuru, nishati, miundo mbinu na maji kwa kuhakikisha kuwa hata kama sehemu nyingine vitu hivyo havipatikani ndani ya EPZs visikosekane.
Akirejea maoni ya OECD alisema huenda uchambuzi wa kutosha kwenye uanzishwaji wa miradi hiyo hapa nchini  haukufanyika.
“Tulichambua watu wanaoingizwa kwenye hizo kanda? Kulikuwa na wawekezaji waliostahili  upendeleo huo? Ni watu waliokuwa na mwelekeo wa kuwa wazalishaji wakubwa ama ni wajanja walichangamka baada ya kusikia kuna mkakati huo kwa kuamini kuwa atanufaika akiingia kwenye kanda hizo?” alihoji.
Alionya kuwa huenda walioingia kwenye eneo hilo  hawakuwa wamebobea pengine hawana sifa zinazotakiwa. Huenda hawana uwezo wala teknolojia ya kuzalisha kwani teknolojia ni ya kwao, haikuwa ndani ya kanda hizo.
Kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuchambua faida na hasara za uwezekaji huu ukibainika kuwa ni gharama zaidi kuwa nazo ni vyema kuachana nazo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment