Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 8 February 2014

PINDA: MIGOGORO YA ARDHI TISHIO LA AMANI YA TAIFA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la KilutheriTanzania, Askofu Alex Malasusa alipokutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika Uzinduzi wa Jukwaa la Ardhi Tanzania.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amelitaka Jukwaa la Ardhi Tanzania kuitazama migogoro ya ardhi kwa mtizamo chanya kwa kuwa inaongezeka na ni viashiria vya kupotea kwa amani ya taifa.

Aidha, amesema umuhimu wa amani kwa taifa ni mkubwa, kwani bila amani hakuna maendeleo.

Pinda alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Jukwaa hilo litakalokuwa chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kushirikiana na serikali na asasi zisizokuwa za kiserikali kwa lengo la kuelimisha jamii na kufanya tafiti juu ya migogoro ya ardhi.

“Suala la migogoro ya ardhi litizamwe kwa mtizamo chanya na wataalamu mbalimbali. Kila kukicha inaongezeka na kulisababishia taifa hasara, ikiwa ni pamoja na watu kupoteza maisha. Naamini jukwaa hili ni suluhisho tosha,” alisema Pinda.

Mwenyekiti wa muda wa Jukwaa hilo, Askofu Stephen Munga, alisema  jukwaa litawaleta wadau kwa pamoja kwa kushirikiana na serikali.

Alisema watafanya tafiti mbalimbali na kuelimisha jamii na kutoa taarifa sahihi kwa kutumia makongamano.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment