Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 12 February 2014

Wafaransa wamkabidhi Kapombe Yanga kwa Sh 154m

Shomari Kapombe.
Na Mwandishi Wetu
KLABU ya AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Ufaransa, hatimaye imetangaza kumuuza beki wake Shomari Kapombe.

Uongozi wa AS Cannes umesema bei ya Kapombe ambaye bado yuko hapa nchini ni euro 70,000 (Sh milioni 154) huku ikitaja majina ya klabu mbili, Yanga na Azam FC wanakaribishwa kuanza mazungumzo.
Awali, gazeti hili lilipata taarifa za ndani kuhusiana na uamuzi huo, lakini uongozi ukawa mgumu kulizungumzia.

Lakini jana mchana, mmoja wa viongozi wa AS Cannes, Pierre Pilorget aliliambia Championi Jumatano kwamba wamefikia uamuzi huo na klabu za Tanzania zilizokuwa zinamtaka zinaweza kufanya mazungumzo na wakala wake au klabu hiyo.
“Waambie Yanga kuwa sasa Kapombe tumemuweka sokoni, wanaweza kumpata na bei ndiyo hiyo. Kama tulivyosema awali wasipite njia za mkato.
“Njia nzuri ni kufika kwetu na kuzungumza, wakiona hawawezi kufanya hivyo wazungumze na wakala wake naye atafika kwetu,” alisema Pilorget.

Alipoulizwa jana kutoka Uholanzi, wakala wake Denis Kadito alisema angependa kuliacha suala hilo lizungumziwe na klabu.
Simba ilimpeleka Kapombe AS Cannes bila ya malipo huku ikusubiri kama atauzwa, itapata asilimia 40 ya mauzo yake.
Championi kilikuwa chombo cha habari kuandika kwamba Yanga na Azam FC walikuwa wakimvizia Kapombe na wengine wamekuwa wakifuatilia kuhusiana na ukweli wa beki huyo ambaye amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ufaransa ingawa hakupata mafanikio.

<gpl>

No comments:

Post a Comment