Hazard (katikati) akishangilia baada ya kutimiza hat trick |
CHELSEA imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle United jioni hii Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, wakati Manchester City ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Norwich City Uwanja wa Carrow Road.
Mabao
ya Chelsea leo yote yametiwa kimiani na Edin Hazard dakika ya 27 pasi
ya Ivanovic, dakika ya 34 pasi ya Samuel Eto'o na dakika ya 63.
Matokeo hayo yanaipandisha kileleni Chelsea ya Jose Mourinho kwa kufikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 25, ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 55 na Man City 54, zote pia zimecheza mechi 25.
Mechi nyingine za leo Liverpool imeichapa 5 - 1 Arsenal, Aston Villa imelala 2-0 mbele ya West Ham United, Crystal Palace imeilaza 3 - 1 West Bromwich, Southampton imetoka 2 - 2 na Stoke Cit na Sunderland imefungwa 2-0 na Hull City.

Alexander Tattery wa Norwich akimdhibiti Stevan Jovetic wa Man City leo CHANZO: BINZUBEIRY |
No comments:
Post a Comment