Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 13 February 2014

SIMBA YAIFUATA MBEYA CITY KWA PIPA

Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic

Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema kuwa hana hofu yoyote na mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City itakayofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Simba ambayo awali ilipanga kwenda Mbeya leo, sasa itaondoka kesho Ijumaa kwa usafiri wa ndege.
Akizungumza na NIPASHE jana mchana, Logarusic, alisema kwamba anaifahamu Mbeya City na mara nyingi mechi zinazohofiwa ndiyo huwa na matokeo mazuri kwake na kwa klabu nyingine.
Logarusic alisema kwa kifupi kwamba anajua katika hatua ya lala salama hakuna mechi rahisi na kikosi chake kimejiandaa kusaka ushindi.
"Kila mmoja anataka ushindi, tunakwenda kutafuta pointi na tuko tayari kwa changamoto zote," Logarusic alisema kwa kifupi.
Kocha huyo aliongeza kwamba muelekeo wa timu hiyo kumaliza katika nafasi mbili za juu utaonekana baada ya mechi ya leo na nyingine mbili watakazocheza dhidi ya Azam na Yanga hapo baadaye.
Naye kocha msaidizi wa timu hiyo, Selemani Matola, alisema jana kwamba kikosi hicho kilitarajiwa kuendelea na mazoezi yake jioni kwenye uwanja wa Kinesi.
Matola alisema kuwa wachezaji watakaokwenda Mbeya watajulikana baada ya mazoezi ya leo jioni.
"Ila tutaenda na wachezaji wachache muhimu, tunafahamu wazi mechi hiyo itakuwa ni ya vuta nikuvute," alisema nahodha huyo wa zamani wa Simba.
Wekundu wa Msimbazi watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa JKT Mgambo walichokipata jijini Tanga wakati Mbeya City wenyewe walipata ushindi wa nyumbani wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani, Morogoro.
Simba iko katika nafasi ya nne kwa pointi 31, tano nyuma ya vinara Azam ambao wamecheza mechi moja pungufu. Yanga wako katika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 35 na Mbeya City wenye pointi 34 wanafuatia.
Wakati huo huo, Simba imeingia makubaliano maalumu na benki ya Posta Tanzania na itakuwa ikitarajia kupata fedha kutoka katika benki hiyo.
CHANZO: NIPASHE     

No comments:

Post a Comment