Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 13 February 2014

KAYA 177 ZAISHI MAPANGONI

Kaya 177 katika wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro zinaishi katika mapango baada nyumba zao kubomolewa huku watoto 350 wakikosa nafasi za kwenda shule baada ya wananchi wa kijiji cha Mbangayao kuhamishwa katika  kijiji hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa ni eneo la hifadhi ya misitu.

Wananchi hao wameamua kuishi katika mapango kutokana na kupinga kuhamishiwa katika Kijiji kipya cha Isaka na kuacha eneo hilo kuendelea kUwa hifadhi ya misitu ya mlima Mbagangayao.
Hali hiyo imeasababisha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kuunda kamati ndogo ya madiwani watano wakiongozana na wataalamu kutoka idara ya elimu, afya na mazingira kwenda katika kijiji  hicho kipya ili kujionea hali halisi.
Akiwasilisha hoja binafsi katika kikao cha baraza la madiwani, Diwani wa Isongo, Henry Balua, alisema kwa sasa wananchi hao hali zao ni mbaya KUtokana na kutoandaliwa miundombinu katika makazi mapya na kuwa hivi karibuni alikwenda katika kijiji  kipya na kuwakuta wakazi hao hawana huduma muhimu zikiwemo, nyumba bora.
Alisema walilazimika kufanya vikao na wananchi hao katika mapango mbayo  zinaishi zaidi ya familia za watu 30 kila pango. Alisema waliondolewa kwa kutumia nguvu kubwa licha YA  wananchi hao walikuwa wakiishi kihalali tangu mwaka 1954.
Alisema ilitangaza katika gazeti la Serikali namba 154 la Mei 17 1991 na kuchukua hekta zote 2245 hata hivyo zoezi hilo halikufanyika hadi  Mei mwaka jana lilipoanza tena baada ya mkuu wa wilaya ya Ulanga kwenda Mbangayao na wataalamu wa misitu na kuwataka wananchi hao kuhama.
Katika barua yake ya Oktoba 5, 2013 yenye kumb.Na.DFM/UL/MZ/FR/VOL.2/18 kwa wananchi wa vitongoji vya Lupanga na Mbangayao, Mkuu huyo wa wilaya  aliwataka kuondoka ndani ya msitu wa hifadhi. Mzelezi kuanzia Oktoba 5, 2013 hadi Novemba 4/ 2013.
Barua hiyo iliendelea kusema kuwa watakaokaidi ilani hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo Balua alisema kuwa kutowatambua wananchi hao ni kosa kwani wapo kihalali eneo hilo na eneo lililotengwa kwa ajili ya msitu wa hifadhi halijaguswa na  kuiomba serikali kuwajengea kwanza miundombinu wananchi hao na kisha kuwalipa fidia.
Hata hivyo diwani huyo alishangaa serikali kupuuza maombi ya wananchi hao na kuamua kuvunja nyumba zao kisha kuwaamisha kwa nguvu bila kuwalipa fidia yoyote.
Alidai kuwa kuna haja kwa halmashauri kupeleka mahema, madawa na chakula kwa wakazi hao vinginevyo  wakiendelea kuachwa hivyo hivyo wana hatari ya kupata magonjwa ya milipuko.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Furaha Lilongeli, alisema kamati hiyo itakapowasilisha majibu itahakikisha inapeleka nguvu ya kuwasaidia wananchi hao
CHANZO: NIPASHE     

No comments:

Post a Comment