Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 19 February 2014

WAZIRI CHIZZA ANENA ARUSHA


Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blog, Arusha

Waziri wa Kilimo ,Chakula na Ushirika Mhandisi, Christopher Chiza amesema kuwa suala la uhaba wa chakula katika kipindi mwaka ujao itakuwa historia kwani wizara yake imejipanga kuongeza ziada ya tani 100,000 ya mazao ya aina yote.

Mhandisi Chiza alisema hayo mara baada ya kukagua mradi wa umwagiliaji maji uliopo Tengeru Wilayani Arumeru Mkoani Arusha,maghala ya Taifa ya nafaka na kutembelea kinu cha iliyokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa{NMC} ambacho kwa sasa kinaendeshwa kwa mkataba na kampuni usagishaji na usambazaji nafaka ya Monaban inayomilikiwa kwa asilimia 100 na mzawa Philemoni Mollel.

Alisema Wizara yake imekuwa ikipanga mipango hiyo kwa maslahi ya serikali na wananchi wake na makakati huo utafanikiwa kwa asilimia mia.

Mhandisi Chiza alisema kutokana na hilo chakula kwa kuanza mwaka ujao kitakuwa cha kutosha kwa asilimia 108 na itafanya mkulima kuuza nje ya nchi ili aweze kujikimu katika masuala yake binafsi.

Alisema hawezi kuwa Waziri wa kilimo,chakula na ushirika kwa kumzuia mkulima kuuza chakula nje la hasha bali yuko kwa ajili ya mkulima kumsaidia kupata mazao ya ziada kwake na kwa nchi na ziada kuuzwa nje kwa faida yake.

Waziri alisema kuwa atahakikisha mkulima anauza mazao nje baad aya ye yeye kutosheka na maghala ya serikali kujaa kila kona kwani kwa sasa serikali ina mpango wa kujenga maghala mengine zaidi kwa jili ya kuhifadhi mazao ya nafaka.

 ‘’Mimi sio waziri Mzigo kama watu wanavyodai bali ni waziri mchapakazi na jamii itanikubali katika muda mfupi ujao katika mkakati wake huo’’alisema

‘’Nimefanya kazi kanda ya kaskazini katika miradi mingi ya kilimo cha uwagiliaji katika miaka ya 1980 ni mtaalamu wa kilimo ninajua ninachofanya wakulima na wananchi iko siku watanikubali na kujua sio waziri mzigo katika wizara hiyo’’alisema

Akizungumzia suala la ombi la Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Monaban kutaka kuuziwa kinu cha NMC Arusha,Waziri Chiza alisema ni suala linalohita Baraka ya kikao cha Baraza la mawaziri.

Waziri Chiza alisema na kumtaka mwekezaji huyo mzawa kuondoa shaka na kumtaka kuendelea kuwekeza kama walivyoingia mkataba na NMC kwa kufanya mambo makubwa zaidi kwa faida ya wakulima kwani serikali haitamwangusha kwani amekuwa akifanya vema sana mpaka sasa.

Alisema kwa kipindi cha mwaka juzi mwekezaji huyo baada ya kukodishiwa kinu hicho na NMC aliweza kufanya vyema katika utoaji wa huduma hiyo ambapo yeye na wawekezaji wengine walipewa mahindi na serikali kwaajili ya kusagisha na kuuza unga kwa bei naafuu ambapo alifanya vyema na taarifa anazo.

“Sisemi hili kwa kuwa upo hapa hapana ila ni kweli kwamba katika wawekezaji waliopewa mahindi ya msaada na serikali ili kusagisha na kuuza unga kwa wananchi kwa bei naafuu wewe ni mmojawapo kati ya waliofanya vizuri kwani wengine walichakachua hivyo nakupongeza”alisema Waziri Chizza.

Kufuatia ombi hilo alisema suala la kukubaliwa au kukataliwa kwa ombi lake hilo halitolewi majibu nay eye binafsi bali ni baraza la mawaziri hivyo atawasilisha ombi hilo kwa baraza hilo mapema iwezekanavyo ili litolewe maamuzi haraka pia.

Alisema hata hivyo hana wasiwasi wa ombi hilo kutokubaliwa kutokana na ukweli kwamba mwekezaji huyo amefanya kazi yake vyema tangu alipokodishiwa kinu hicho mbali na mtaji mkubwa aliowekeza wa zaidi ya bilioni tisa katika ununuzi wa mitambo mipya hata kabla ya kujua atapewa kinu hicho au laa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban Philemon Mollel alisema kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia 100 na wazawa hivyo kuitaka serikali kupitia kwa waziri huyo kuacha kusikiliza propaganda zinazodai kuwa kampuni imewahi kuuza hisa na ina mtaji wa kutosha.

Pia alisema kampuni ina mpango wa uwekezaji wa muda mfupi na mrefu ambapo kwa uwekezaji mfupi ina mpango wa utengenezaji wa maji safi na salama,juisi za matunda ikiwa ni njia ya kuwaokoa wakulima dhidi ya hasara wanayoipata kwa matunda yao kuozea mashambani.

Pia kampuni ina mpango wa kuwoka mikate yenye ubora ambayo itauzwa kwa bei naafuu kwa ajili ya wananchi ambapo tayari mipango imeshaandaliwa na kwamba inatarajiwa hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu bidhaa itakua sokoni.

Katika uwekezaji wa mura mrefu alisema kampuni inataraji kuanza utengenezaji wa vifungashio vya bidhaa mbalimbali kwaajili ya kampuni pamoja na wajasiriamali wadogo ili kuondokana na kero kwao ambapo walikua wakilazimika kuagiza toka nchi jirani ya Kenya kwa bei ya juu.

Aidha alisema katika kukuza kipato cha wakulima kampuni imeanza kuwahamasisha katika kilimo cha Mahindi,Mtama,Balee,Mbaazi na ulezi kwa kuwahakikishia soko na uhakika na kuondokana na soko la ubabaishaji hivyo kampuni pia iko katika mkakati wa ujenzi wa maghala ya kutosha.

Waziri Chizza alikua mkoani Arusha kwa ziara ya siku tatu kwaajili ya kukagua mashamba yenye mgogoro wilayani Arumeru,uzinduzi wa kilimo cha umwagiliji kupitia mfereji wa Mapama pamoja na kuzungumza na uongozi na wafanyakazi wa kinu cha NMC jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment