Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa hali ya hewa kutoka sekta mbali mbali katika mkutano wa wadau wa utabiri wa mvua za msimu wa MASIKA kwa mwezi Machi mpaka Mei 2014.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA
YA HALI YA HEWA
MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YAKUTANA NA
WADAU WA SEKTA MBALI MBALI KUJADILI UTABIRI WA MVUA ZA MSIMU KWA MWEZI
MACHI-MEI (MASIKA)TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Kila mwaka mwezi
Februari kabla ya kutoa utabiri wa msimu Mamlaka hukutana na wadau wa sekta
mbali mbali nchini ili kujadili utabiri wa msimu huo wa mvua za MASIKA kwa kipindi cha miezi ya
Machi hadi Mei na kuwapa wadau nafasi ya
kuchangia namna utabiri huo utakavyotumika katika sekta zao.
Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes
Kijazi alisema mchango wa wadau katika matumizi ya utabiri ni wa
muhimu kwani utabiri unaotolewa hauwezi kuwa na manufaa endapo wadau kutoka
sekta mbalimbali hawatautumia katika kuboresha shughuli zao.Aliongeza kusema
kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hali ya hewa imekuwa ikibadilika sana
(climate variability) hivyo akasisitiza kwamba ni muhimu sekta mbali mbali za
kiuchumi na kijamii zikatilia maanani taarifa za hali ya hewa katika mipango ya
shughuli zao.
Mshiriki kutoka Wizara
ya Kilimo na usalama wa chakula (MAFS-NFRA) Bw. Joseph Peter Oganga alieleza umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta
mbalimbali hususan kwenye upatikanaji wa chakula kwa kupanga namna ya kutumia
utabiri katika kupanga uzalishaji wa mazao husasn katika kipindi hiki ambacho
dunia nzima ikishuhudia mabadiliko ya tabia nchi .
Mshiriki kutoka Timu
ya Wataalamu wa Kukabiliana na Maafa Mkoa wa Dar es salaam – DARMAERT(Dar es
salaam Multi-Agency Emergency Response Team) Bw. Amini Mshana kwa upande wake
alisema mikutano hii inasaidia sana kujiandaa na maafa ili kupunguza athari
zinazoletwa na maafa akitolewa mfano mafuriko,mlipuko wa magonjwa n.k
Kwa upande wa sekta ya
habari, Mwakilishi kutoka Magic radio Bw Salum Mkambala alisema wanahabari ndio
kiunganishi cha jamii hivyo ni muhimu kujua changamoto zinazoikabili TMA katika
usambazaji wa taarifa za hali ya hewa na kutafuta muafaka huku wakitumia fursa
hii kuwaomba wadau wengine kutoa taarifa zinazoeleweka kwa kila mwana jamii
hususan zile zitokanazo na hali ya hewa
Taarifa za hali ya
hewa ni muhimu katika sekta ya afya kwani magonjwa yanayohusiana na hali ya
hewa ni mengi kama vile malaria na kuharisha, alisema mshiriki kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii bw. Makono Andrew.
Wadau walioshiriki na
kutoa michango yao katika mkutano huo ni kutoka Wizara ya Afya (MNCP)
Makono Andrew na Amina Kingo (Epidemiology), Wizara ya Maji Mwasiti Rashid,
Wizara ya Mifugo Lugendo Bunto,RedCross, TBC Mwasu Sware, Salum Mkambala (Magic
FM),DARMEART Amini Mshana, Wizara ya Uchukuzi Shinja Shaffih,Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa DSM Boniface Chija,Ofisi ya Mipango Josiah Mwabeza,Wizara ya Kilimo Joseph
Ogonga, Wizara ya Nishati na Madini Innocent Makomba,Climat Consult Philbert
Tibaijuka, Ofisi ya Waziri Mkuu (maafa) Edward Boniface,CWCAR-DSM Dkt Mohamed
Mhita
Akifunga mkutano
huo Dkt. Agnes Kijazi alisema utabiri wa
msimu wa MASIKA utatolewa rasmi tarehe
27 Februari 2014.
IMETOLEWA NA MONICA
MUTONI;OFISI YA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment