Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 19 February 2014

DKT MUKANGARA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUZINGATIA MAUDHUI

Dk. Fennela Mukangara

Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blogspot, Arusha

WAZIRI wa habari, vijana  michezo na utamaduni, Dr. Fenella Mukangara amevitaka vyombo vya mawasiliano kuzingatia maudhui yaliyowekwa ili kuwawezesha watanzania kuepukana na changamoto wanazokutana nazo katika uhamaji wa mfumo wa analojia kwenda digitali.
Aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa siku nne uliowashirikisha wadau kutoka nchi zaidi ya mia moja kutoka jumuiya ya madola katika kujadili changamoto ambazo nchi zinakumbana nazo katika mfumo huo wa kuhama analojia kwenda digitali.
Alisema kuwa,ni vyema vyombo hivyo vikasimamia maudhui kwa kuwa zipo baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika mfumo huo, hali ambayo inawafanya watanzania kukosa huduma zao za msingi.
"Mkutano huu wa kimataifa ni muhimu sana kwani tunaangalia tangu kufunguliwa kwa mfumo wa digitali wananchi wamekutana na changamoto gani, na ni maudhui gani yabebwe katika kuzikabili changamoto hizo na kwa kufanya hivyo tutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea na kwa wakati muafaka," alisema Mukangara.
Aidha alisema kuwa, kuhamia katika mfumo huo, kutawezesha sio wananchi kubadili uzoefu pekee wa kuangalia mitandao ya nje bali hata kutaharakisha maendeleo katika nchi zetu na hatimye kuondokana na changamoto mbalimbali walizokuwa wakikabiliana nazo kwenye mfumo wa analojia.

No comments:

Post a Comment