TAARIFA KWA UMMA
UPOTOSHWAJI NA PROPAGANDA CHAFU DHIDI YA CHADEMA/UKAWA NA KIKUNDI KILICHOJIVIKA VYEO HEWA
Zimetolewa
taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mtu anayejitambulisha
kwa jina la Fikiri Migiyo na ambaye amejitambulisha pia kama Mwenyekiti
wa Mabaraza ya kanda ya Ziwa Magaharibiinayojumuisha mikoa ya Mwanza,
Simiyu, Kagera na Geita akipinga kuundwa kwa umoja wakutetea katiba ya
wananchi (UKAWA)
Aidha mtu huyo
anayejitambulisha na BAVICHA ameenda mbali kwa kutoasiku 14 kwa CHADEMA
kujiondoa kwenye UKAWA na pia kulaani kitendo cha UKAWA kususia Bunge la
Katiba.
Barazala Vijana wa Chama cha
Demokrasisa na Maendeleo (CHADEMA) linapenda kuufahamisha umma wa
Tanzania na wapenda mabadiliko mambo yafuatayo:-
1. BAVICHA haina kiongozi wa jina hilo la Fikiri Mayingi kwa Mkoa wa Geita
2.
Katika muundo wa chama na Mabaraza yake hakuna cheo kinachoitwa
Mwenyekiti wa makatibu wa Mabaraza kwa Kanda. Hivyo mtu huyo aliyetoa
tamko hilo amejipachika cheo hicho ili kukidhi hajana matakwa yake
binafsi kwa nia ovu ya kuichafua CHADEMA
3.
Pia ni muhimu umma ukaelewa kuwa Muundo wa uongozi wa BAVICHA na hata
mabaraza mengine ya chama unakomea kwenye ngazi ya mkoa na kisha Taifa
mpaka hapo muundo wa kanda utakapohuishwa kwenye mfumo wa baraza kuanzia
kwenye chaguzi zijazo. Hivyo kilichotolewa kwa umma ni cha kuupuuza.
4.
BAVICHA haijawahi kufanya uchaguzi kwa mikoa yote mipya ya Geita,
Simiyu, Njombe na Katavi hivyo kusema kwamba yeye ni mwenyekiti wa
makatibu wa mabaraza ya chama kwa mikoa tajwa ni hila za kisiasa
zinazoendeshwa na kundi la vijana waasi wanaoendeshwa na kivuli cha mtu
badala ya itikikati, falasafa na sera za CHADEMA.
5.
Aidha, mkoa wa Simiyu uliotajwa kwenye taarifa ya mpotoshaji huyo kuwa
ipo kanda ya Ziwa Magaharibi si sahihi licha ya kwamba tu haina uongozi
wa BAVICHA zaidi ya Kamati ya Msukomo kwa masuala yote ya kichama
ikiwemo mabaraza. Mkoa wa Simiyu uko kanda ya Ziwa Mashariki na si ziwa
Magharibi kama alivyosema mpotoshaji.
6.
Ieleweke kuwa, Hakuna Mwanachadema mwenye akili timamu anayeweza kupinga
uwepo na shughuli za UKAWA kwenye mchakato huu wa katiba mpya, umoja
unaobeba maslahi mapana ya taifa letu, umoja unaotete maoni ya wanachi
dhidi ya wapinga maoni ya wananchi anaye jitambullisha kama
mwanachadema, wanaopinga maoni ya wananchi na rasimu ya katiba mpya
wanajulikani.
7. Aidha, hakuna mwanachadema/
BAVICHA mwenye akili timamu anayeweza kuunga mkono vitendo vya kibaguzi,
kidini na kikabila, achilia mbali matusi na vitisho vilivyofanywa na
Serikali na Wabunge wa CCM kwenye bunge la katiba kwa kupinga kitendo
cha UKAWA kutoka nje ya bunge hilo. Mwanachadema anayeweza kutetea
vitendo hivyo anajinasibisha kwa utambulisho wa CHADEMA lakini si
mwanachadema.
8. Baraza la vijana la chama cha
Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) linawaomba wanachama na Watanzania
kuwapuuza vijana hao wanao tumika kwa kujipachika vyeo visivyokuwepo
hata kwenye Katiba ya Chama na Mabaraza yake ili kukidhi adhima na nia
ovu ya kuchafua taswira nzima ya CHADEMA.
9.
BAVICHA daima itaendelea kuunga mkono juhudi za UKAWA za kupigania
upatikanaji wa Katiba bora ya Wanatanzania inayotokana na maoni yao
wenyewe.
Imetolewa leo Jijini Dar es salaam na:
Deogratias Munishi
Katibu Mkuu - BAVICHA
No comments:
Post a Comment