Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 23 May 2014

CHADEMA YA MALAWI KIDEDEA, CCM YA MALAWI TAABAN!

Rais Joyce Banda wa Malawi

CHADEMA ya Malawi, Democratic Progressive Party (DPP), kupitia kwa mgombea wake Profesa Peter wa Mutharika inaelekea kupata ushindi wa kishindo, huku mgombea wa CCM ya Malawi, People’s Party (PP), Bi Joyce Banda, akiangukia pua kwa kuendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya mgombea wa Chama cha CUF ya Malawi, Malawi Congress Party (MCP), Bw Lazarus Chakwera anayeshika nafasi ya pili.
 
Bi banda hajafanya lolote la maana kwa nchi na wananchi wa Malawi tangu ashinde uchaguzi uliopita. Alichofanikiwa tu ni kuwatisha watanzania kwa kutaka kuwanyang’anya ziwa, lakini ktk utawala wake uchumi wa Malawi umezidi kushuka na maisha ya wananchi yamekuwa duni zaidi kuliko ilivyokuwa katika utawala wa Rais aliyepita. Ni bora huyu king’ang’anizi ameondoka, sasa walau watanzania tutapumua na presha ya kunyang’anywa ziwa.
 
Bi Banda anatapatapa kwa kudai kwamba kura zimeibiwa, akitaka uhesabuji kura urejewe. Awali mashine za kieletronic zilikuwa zikitumika kuhesabu kura (kama zile zilizotumika Kenya) lakini zilifeli na kura zikaanza kuhesabiwa kwa mikono.
 
Mwenyeketi wa tume ya uchaguzi ya Malawi, Jaji Maxon Mbendera, ametupilia mbali maombi ya Banda kutaka kura zihesabiwe upya.
Awali Bi Banda alikimbilia mahakamani kuweka pingamizi ili kuzuia matokeo yasitangazwe lakini mahakama yametupilia mbali maombi yake. Baada ya hapo ndipo akaanza kuhaha kwa kuitisha press conference akitaka wamalawi wamuonee huruma kwa kilio chake cha kushindwa. Mbinu zote hizo zimegonga mwamba.
 
Bi Banda pia amefanya uhuni kwa kutuma majeshi kuvamia nyumbani kwa Prof Mutharika siku ya Jumatano. Mutharika amelaani uvamizi huo na kuuita ni ‘ubakaji wa demokrasia’. Walinzi wa nymbani kwake waliwakatalia wanajeshi hao kuingia nyumbani kwa kuwa hawakuwa na kibali ya kupekua nyumbani kwa bosi wao.
 
Aidha, Bi Banda alimfanya sarakasi Prof Mutharika kwa kuwatumia polisi kuvamia jengo la kujumuishia kura kwa lengo la kuleta vurugu ili apate kisingizio kizuri cha kurudiwa kuhesabiwa kura au kurudiwa uchaguzi mzima. Ujanja huu umeshtukiwa na wanamalawi ambao wamechoshwa na utawala wa kichokozi wa Bi Banda.
 
Wakati hayo yakitokea, Waziri mmoja wa chama cha People’s Party (PP), Bw Godfrey Kamanya amejipiga risasi na kufa papo hapo baada ya kushindwa katika jimbo la Msozi Kaskazini alilokuwa akiliongoza katika muhula wa bunge auliopita.
 
Ushindi wa CHADEMA ya Malawi (DPP) ni dalili njema kwa mageuzi barani Africa na ishara nzuri kwa CHADEMA ya Tanzania kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwaka 2015. Natumaini upepo wa mageuzi ambao umeanzia India (PJP) na kuvuma hadi Malawi (DPP) utafika Tanzania na hatimaye watanzania watakombolewa kutoka ukoloni mamboleo.
 

Source: Nyasa Times/Mabadiliko Forums

No comments:

Post a Comment