MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
TAARIFA KWA UMMA
Mfuko
wa Pensheni wa PSPF unapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa, hivi
karibuni kumekuwa na watu au kikundi cha watu wanaosambaza taarifa
potofu kwa wanachama wa PSPF kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi
kwa nia ya kuwatapeli.
Taarifa hizo zinazotolewa siyo sahihi na PSPF inawaomba wanachama wake kuchukua tahadhari dhidi ya
ujumbe huo wa kupotosha unaosambazwa kwa njia ya simu na watu au kikundi cha watu wakidai kuwa ujumbe huo unatoka PSPF.
PSPF
inatoa huduma mbalimbali kwa wanachama wake bila sharti lolote wala
malipo ya namna yoyote. Ujumbe wowote unaomtaka mwanachama kutuma fedha
kwa ajili ya kulipia huduma yoyote inayotolewa na Mfuko siyo sahihi na
ujumbe wa namna hiyo hautolewi na PSPF. Hivyo, ninawaomba wanachama wa
PSPF kuwa makini na ujumbe huo unaosambazwa na watu wachache ambao
wanataka kuuchafua Mfuko na kujinufaisha kwa njia zisizo halali.
Iwapo
itatokea mwanachama amepata ujumbe wenye utata, tafadhali piga simu
katika Kituo cha Huduma kwa Wateja wa PSPF kwa kutumia namba 022 5510400
au fika katika ofisi ya PSPF iliyopo karibu nawe au toa taarifa kituo
chochote cha polisi kilicho karibu nawe kwa hatua stahiki.
Taarifa hii imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Makao Makuu, Golden Jubilee Towers, S. L. P. 4843, Dar-es-Salaam.
Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6
Nukushi: +255222120930
Barua pepe: pspf@pspf-tz.org
Tovuti: www.pspf-tz.org
@Pspf_Tanzania
No comments:
Post a Comment