Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kwenye mkutano wa wabunge ambapo waziri wa fedha aliwasilisha mapendekezo na mwelekeo wa bajeti ya serikali kwa mwaka fedha 2014/15, Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao .
Dar es
Salaam. Serikali imetoa mwelekeo wa Bajeti ya
mwaka wa fedha wa 2014/15 kuwa ni Sh19.6 trilioni, ikilinganishwa na Sh18.2 za
Bajeti iliyopita.
Vipaumbele vya Bajeti hiyo ni kuendeleza
Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioanza mwaka 2011 na Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) ambao unajumuisha maeneo sita ya kitaifa ya kilimo, elimu,
maji, utafutaji wa rasilimali fedha, nishati, uchukuzi na uboreshaji wa
mazingira ya kufanyia biashara.
Katika kuhakikisha inakusanya fedha za
kutosha, Serikali imeahidi kuunda kikosi kazi cha kufuatilia mapato yote
yanayotoka halmashauri zote nchini ili kuondoa visingizio vilivyojitokeza
wakati wa ufuatiliaji wa mapato.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Fedha,
Saada Mkuya wakati akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti hiyo kwa kamati zote za
Bunge, Dar es Salaam.
Alisema matumizi ya kawaida kwa mwaka
ujao wa fedha yanalenga kufanikisha mambo 20 muhimu, yakiwamo Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwaka 2014, Uchaguzi Mkuu 2015, kukamilisha mchakato wa
Katiba na nyongeza ya mishahara na kulipa kwa wakati.
Mkuya alisema makadirio ya matumizi ya
maendeleo ni Sh7.7 trilioni sawa na asilimia 39 ya matumizi yote ya Serikali.
Kati ya fedha hizo, miradi ya maendeleo
imetengewa Sh5.4 trilioni sawa na asilimia 27 na matumizi mengine ya maendeleo
ni Sh2.2 trilioni.
Utegemezi
Mkuya alisema katika mwaka unaomalizika,
Serikali ilipanga kukopa Dola 700 milioni za Marekani sawa na Sh1.1 trilioni na
kati ya kiwango hicho, iliambulia mkopo wa Dola 259 milioni hivyo kuweka nakisi
ya Dola441.
Alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015,
Serikali imekusudia kukopa Sh4.2 trilioni kutoka vyanzo vya mapato vya ndani na
nje ili kuziba pengo la mapato.
Misaada na pato la taifa
Katika mwaka wa 2013/2014, Serikali
ilipokea misaada ya Sh1.1 trilioni kutoka kwa washirika wa maendeleo ikiwa ni
asilimia 50 ya ahadi ya Sh2.3 trilioni, hivyo kuweka nakisi ya Bajeti ya Sh1.2
trilioni.
Akiwasilisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo
wa Taifa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Stephen Wassira alisema deni la Taifa limefikia Sh27.04 trilioni kutoka Sh24
trilioni na kufafanua kuwa ongezeko la deni hilo limetokana na mikopo mipya ya
kibiashara na ya masharti nafuu.
Ukusanyaji mbovu wa mapato
Akizungumzia ukusanyaji wa kodi, Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda alisema kumekuwa na matatizo katika ukusanyaji wa mapato ya
ndani, hasa yasiyotokana na kodi.
“Tumepata changamoto na tunajiuliza kwa
nini hatufikii malengo, lakini tunaamini kwamba tukijipanga vyema kwenye
halmashauri zetu kwa kuzibana vyema, tutaweza kupiga hatua nyingine kutoka hapa
tulipo,” alisema.
CHANZO, MWANANCHI
No comments:
Post a Comment