Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday, 1 July 2014
'WATIENI MOYO WALIOFELI KIDATO CHA NNE'
Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot
ARUSHA: SERIKALI imetakiwa kuweka utaratibu maalumu wa kuhakikisha kuwa haiwatupi wanafunzi waliofeli kidato cha nne na badala yake wanawatafutia njia mbadala ikiwa ni pamoja na kuwakusanya tena kwa mara nyingine na kuwapa maarifa mapya.
Endapo kama Serikali itafanya hivyo basi taifa la Tanzania litaweza kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na kidato cha tano na sita ambacho nacho ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule ya msingi na sekondari ya Arusha Modern, Philiph Wasike wakati akiongea na wanafunzi wazazi na walezi kwenye maafali ya 12 ya kidato cha nne shule hiyo ambayo yalifanyika juzi jijini hapa.
Wasike alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi ambao wanafeli kidato cha nne wanaonekana kama hawana maana tena mbele za jamii wakati kuna sababu mbalimbali ambazo zinapelekea wanafunzi hao kufeli.
Alifafanua kuwa sababu hizo zinatakiwa ziweze kuangaliwa lakini pia serikali itunge utaratibu maalumu wa kuwakusanya walioshindwa mthiani na kisha kuwapa hata nasaha ambazo zitaweza kuwafanya wasikate tamaa.
"Kufeli kidato cha nne sio kufeli maisha bali sisi kama jamii lakini pia sisi kama Serikali tunatakiwa kuwaonesha upendo wanafunzi hawa na mwanafunzi ambaye ana moyo wa kuendelea huwa anajionesha tu na kama tukifanya hivi idadi ya wasomi wa vyuo vikuu itaongezeka maradufu tofauti na sasa ambapo idadi ya wasomi wa vyuo vikuu hapa nchini bado hairidhishi hata kidogo," aliongeza Wasike.
Kutokana na hilo alisema kuwa shule yake tayari imeshaweka utaratibu wa kuwatia moyo wale ambao wamefeli kidato cha nne ambapo wanapewa mafunzo maalumu kwa ajili ya kufanya vema zaidi mthiani wa taifa jambo ambalo wamefanikiwa kwa kiwango cha juu sana.
"Hawa wanafunzi ambao sisi tumeanza nao toka mwaka 2011 kwa kweli wamefanya vizuri sana na wamepata alama za juu sana kwenye mthiani yao ya taifa sasa huu mpango mimi naweza kusema kuwa unaweza kuwasaidia walio wengi kama utaigwa ila hata wakitumia shule yetu sisi tupo tayari kuwalea hawa ambao wamefeli kidato cha nne na wakaenda kidato cha tano tena kwa raha sana"aliongeza Wasike.
Alihitimisha kwa kusema kuwa bado shule hiyo inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuweza kuhakikisha inapandisha elimu ya Tanzania ili iweze kufika katika viwango vya kimataifa kama zilivyo nchi
zilizoendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment