BUNGE MAALUM LA KATIBA LIKAE KWA
WIKI MBILI NA SIO MIEZI MIWILI
TAMKO LA JUKATA KUHUSU HAJA YA
RATIBA MPYA YA
MCHAKATO WA KATIBA MPYA TANZANIA
1.0.
UTANGULIZI
Tangu tarehe ya awali
ya ratiba ya Mchakato wa Katiba Mpya Tanzania ipite bila kuipata Katiba,
kumekuwa na ukimya wa muda mrefu bila mwongozo wowote madhubuti juu ya tarehe
mpya za hatua zinazofuata za Mchakato huu adhimu na muhimu wa ustawi wa
demokrasia, utawala bora, uwajibikaji na mshikamano ndani ya Nchi yetu. Ukimya
huo umeleta ombwe kubwa katika Mchakato wenyewe na kusababisha kila mtu kusema
lile aliloweza kusema huku kuhitilafiana baina ya makundi mbalimbali ndani na
baina ya vyama vya Siasa na Makundi mengine ya Kijamii. Kwa uchunguzi wa
JUKATA, hata ufa wa Mchakato kati ya wanaopendelea muundo wa Muungano wa
Serikali mbili na wale wanaotaka serikali tatu ni sehemu ya mivutano ya Kisiasa
inayotokana na wanasiasa kuendelea kujipima umaarufu wao kwa kutumia Katiba
Mpya. Kukosekana kwa ratiba Mpya ya Mchakato pia kulipelekea mfarakano ndani ya
Bunge Maalum baina ya makundi ya vyama vya Siasa ya UKAWA na Tanzania Kwanza
huku kila upande ukijaribu kuitazama Katiba mpya kwa minajiri ya kufanikisha au
kukwaza ushindi wao katika uchaguzi Mkuu ujao wa Mwakani, 2015.
Kutokana
na ukweli kwamba muda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 umekaribia sana,
joto la kisiasa linazidi kupanda na tayari Taifa linakabiliwa na michakato
mikubwa sita ya kitaifa katika kipindi kifupi cha miezi 15 tu iliyobaki hadi
mwishoni mwa Oktoba 2015 ambapo ndipo Uchaguzi Mkuu utalazimika kufanyika kwa
kuwa muda wa kukaa madarakani kwa viongozi wetu wa kuchaguliwa serikalini na
Bungeni utakuwa umekwisha kikatiba. Michakato hiyo ni pamoja na:-
i)
Uandikishaji wa vitambulisho wa Taifa
unaofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ulioanza mwaka 2013 na
mpaka sasa umefanyika katika mikoa ya Dar Es Salaam, Zanzibar na Pwani pekee,
huku Mikoa ya Lindi na Mtwara ikitarajiwa kuanza zoezi hilo mwezi mmoja ujao.
Hadi sasa, hata theluthi moja ya nchi haijafikiwa na zoezi hilo na bado yapo
mategemeo kuwa zoezi hili litakamilika mapema mwaka 2015, kwa mujibu wa ndoto
za NIDA.
ii)
Uchaguzi wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika Kisheria mwezi Oktoba 2014 na ambao kwa jadi husimamiwa
na ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), huku
ukitanguliwa na uandikishaji wapiga kura unaojitegemea.
iii)
Uandikishaji upya wa wapiga kura kwa
mfumo wa kielektroniki yaani Biometric Voter Registration (BVR), unaotarajiwa
kufanyika kuanzia mwezi Septemba 2014 kwa awamu za kikanda ukisimamiwa na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Uandikishaji huu umepangwa kufanyika kwa siku
angalau 14 kila kituo kwa kila Kanda, labda kukiwa na ulazima wa kuongeza muda.
iv)
Upigaji wa kura ya maoni kuamua hatma ya
Katiba Mpya unaofikiriwa kufanyika mwezi Machi 2015 na kuendeshwa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kabla ya uchaguzi huo, kutakuwa na muda wa kuendesha
elimu ya uraia na elimu ya mpiga kura ambayo hata hivyo inaonekana kutopewa
muda na kipaumbele cha kutosha katika mipango rasmi ya Mchakato huo. Aidha, kwa
mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013 kutapaswa kuwa na
muda
wa kufanya kampeni kwa makundi ya Kamati zitakazojisajili ama kupigia debe kura
ya NDIYO au kura ya HAPANA.
v)
Uhakiki wa daftari la kudumu la Wapiga
kura unaofikiriwa kufanyika mnamo mwezi Juni/Julai kama sehemu ya kutimiza
matakwa ya sheria za Uchaguzi zinazotaka daftari hilo kuhakikiwa mara mbili
ndani ya miaka mitano kati ya uchaguzi mmoja na mwingine. Lengo la uhakiki huu
itakuwa ni kuondoa wafu katika daftari pamoja na kushughulikia waliopoteza kadi
za mpiga kura.
vi)
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwezi Oktoba 2015, kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa
Zanzibar, Wabunge wa Bunge la Tanzania na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar pamoja na Madiwani katika Halmashauri zote za Tanzania Bara.
Kutokana na na
michakato na mambo hayo makuu sita muhimu hapo juu ambayo yanatakiwa kufanyika
ndani ya miezi 15 tu ijayo huku mengine yakiratibiwa na kuendeshwa na taasisi
zilezile na kuwahusisha wananchi walewale na rasilimali za Taifa hilihili
ambazo ni finyu JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunapendekeza masuala muhimu mawili
kama hatua ya kupunguza matumizi mabaya ya muda, vifaa na rasilimali fedha
tukiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa mazoezi haya pia :-
a) Kuahirisha
uchaguzi wa serikali za mitaa ili ufanyike pamoja na uchaguzi mkuu mwezi Oktoba
2015 na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) kwa kutumia daftari la
Kudumu la Mpiga kura watakaloliandaa mwaka huu 2014 na kulihakiki katikati ya
mwakani 2015.
b) Kusimamisha
mchakato wa kuandika katiba mpya mpaka mara baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.
c) Kwa
sababu ya pendekezo (b) hapo juu, kufupisha Mkutano ujao wa Bunge Maalum la
Katiba unaoanza tarehe 05 Agosti 2014 mjini Dodoma kutoka siku sitini (60)
alizowaongezea Mheshimiwa Rais,Bunge hilo likutane kwa kipindi cha wiki mbili
pekee ili kufanya kazi moja tu muhimu ya kujadili, kuridhia na kupendekeza
ratiba mpya ya Mchakato
wa Katiba Tanzania. Ratiba hii
itapaswa kuwasilishwa na serikali kama
Rasimu
ya Ratiba baada ya HOJA MAHSUSI ya kulitaka Bunge Maalum kupokea na kujadili
Rasimu ya Ratiba Mpya ya Mchakato wa Katiba Mpya Tanzania. Hoja Mahsusi inaweza
kutoka serikalini au kutolewa na Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum. Baada ya
kutolewa hoja hiyo mahsusi, Waziri mwenye dhamana ya Mchakato wa Katiba
atawasilisha RASIMU YA RATIBA MPYA YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA TANZANIA. Hoja
hiyo itajadiliwa kwa siku zisizozidi tano na ratiba kupitishwa kama pendekezo
kwa Bunge la Tanzania ambalo ndilo litakuwa na Mamlaka ya kupokea na kupitisha
hoja hiyo kama sehemu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
83 (kama ilivyorejewa hadi mwaka 2014).
2.0.
PENDEKEZO LA RATIBA MPYA YA
MCHAKATO WA KATIKA MPYA TANZANIA
NAMBA
|
SHUGHULI
|
|
MUDA
|
|
|
|
|
1
|
Bunge Maalum la
|
Katiba
kukutana na
|
05 – 15 Agosti,2014
|
|
kupokea, kujadili na kuridhia
hoja ya haja
|
|
|
|
ya RATIBA MPYA YA MCHAKATO
|
|
|
|
WA KATIBA TANZANIA
|
|
|
|
|
|
|
2
|
Bunge Maalum la
|
Katiba
kuahirishwa
|
16 Agosti, 2014
|
|
rasmi hadi baada ya Uchaguzi
Mkuu wa
|
|
|
|
2015
|
|
|
|
|
|
|
3
|
Bunge la Jamhuri
|
ya
Muungano wa
|
Novemba, 2014
|
|
Tanzania kupokea rasmi HOJA ya
|
|
|
|
pendekezo la kuahirishwa kwa
Mchakato
|
|
|
|
wa Katiba Mpya hadi baada ya
Uchaguzi
|
|
|
|
Mkuu, 2015 na kupokea Muswada
wa
|
|
|
|
Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya
|
|
|
|
Katiba, 2014 ikiwemo kuingiza
ratiba
|
|
|
|
(roadmap) mpya katika Sheria.
|
|
|
|
-
Muhimu pia kurejesha kifungu cha
|
|
|
|
37
cha Sheria ya Mabadiliko ya
|
|
|
|
Katiba
hadi 2012 kuibakiza Tume
|
|
|
|
katika wajibu
|
wa
kuwepo katiba
|
|
|
|
|
|
Bunge Maalum la Katiba kukutana
kwa
|
Novemba
|
–
|
Disemba,
|
|||
|
ajili ya kuendelea kujadili
Rasimu ya
|
2016
|
|
|
||
|
Katiba Mpya iliyoandaliwa na
Tume ya
|
|
|
|
||
|
Mabadiliko ya Katiba, 2013
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|||
8
|
Bunge la Katiba Kupitisha
katiba mpya
|
|
Januari-Juni, 2017
|
|||
|
|
|
|
|||
9
|
Wananchi kupiga kura ya maoni
|
|
Julai – Novemba,2017
|
|||
|
|
|
||||
10
|
Katiba mpya kutangazwa, kutiwa
saini na
|
1 Januari,2018
|
||||
|
kuzinduliwa rasmi
|
|
|
|
|
|
|
|
|
||||
11
|
Kutunga na kurekebisha sheria
50 kusaidia
|
Januari- Juni,2018
|
||||
|
utekelezaji wa Katiba Mpya
|
|
|
|
|
|
|
|
|
||||
12
|
Kutunga katiba ya Tanganyika na
|
Julai-Desemba, 2018
|
||||
|
Mabadiliko makubwa katika
Katiba ya
|
|
|
|
||
|
Zanzibar
|
|
|
|
|
|
|
· Kuunda Kamati
ya
|
Mabadiliko
|
ya
|
|
|
|
|
Katiba
|
|
|
|
|
|
|
· Kukusanya
maoni ya wananchi
|
|
|
|
|
|
|
· Kuunda bunge
la katiba
|
|
|
|
|
|
|
· Kupitisha
katiba
|
|
|
|
|
|
|
· Kupiga kura
ya maoni
|
|
|
|
|
|
|
· Kutangaza
katiba mpya
|
|
|
|
|
|
13
|
Ukamilishaji wa uundaji vyombo
muhimu
|
Januari- Oktoba,2019
|
||||
|
vya Kikatiba na Kisheria kwa
mujibu wa
|
|
|
|
||
|
Katiba Mpya
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
||
14
|
Uundaji upya wa Majimbo ya
uchaguzi na
|
Novemba
|
–
|
Disemba,
|
||
|
taratibu mpya za uchaguzi
|
|
|
2019
|
|
|
|
|
|
||||
15
|
Uchaguzi Mkuu
kama sehemu ya
|
Agosti-Oktoba,2020
|
||||
|
utekelezaji wa Katiba Mpya
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
||
16
|
Marekebisho ya kisheria
kulingana na
|
Januari
|
–
|
Disemba,
|
||
|
matatizo yaliyojitokeza
|
wakati
|
wa
|
2021
|
|
|
|
uchaguzi Mkuu 2020
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
3.0.
MAPENDEKEZO JUU YA HAJA YA
MABADILIKO (MINIMUM REFORMS) YA MASHARTI MBALIMBALI YANAYOHUSIANA NA UCHAGUZI
KATIKA KATIBA YA TANZANIA NA KATIBA YA ZANZIBAR PAMOJA NA SHERIA ZA UCHAGUZI
Kutokana na hoja yetu
ya haja ya kusogeza uchaguzi wa serikali za Mitaa ili ufanyike wakati mmoja na
Uchaguzi Mkuu, hoja nyingine ya kuahirisha Mchakato wa Katiba Mpya hadi baada
ya uchaguzi Mkuu ujao, ipo haja ya kufanyika mabadiliko kwenye Masharti
mbalimbali ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Katiba ya Zanzibar
ya mwaka 1984 na Sheria kadhaa za uchaguzi na zile zinazohusu usimamizi na
ulinzi katika mazoezi ya uchaguzi ili kupunguza au kuondoa kabisa malalamiko ya
wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya Siasa juu ya usimamizi, uratibu na
uendeshaji wa zoezi zima la uchaguzi nchini. Katika kufikia azma hiyo, JUKATA
tunapendekeza yafuatayo:-
3.1.
MABADILIKO KATIKA BAADHI YA
MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977
· Kubadili
muundo na uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
·
Kuingiza
mgombea binafsi katika chaguzi za ngazi zote
3.2.
MABADILIKO KATIBA BAADHI YA
MASHARTI YA KATIBA YA ZANZIBAR, 1984
· Kutazama
upya maeneo yanayokataza ufunguaji wa Mashauri ya rufani kwa mambo yanayohusu
haki za binadamu katika uchaguzi na ambayo yamekosa majibu ndani ya ngazi zote
za mahakama za Zanzibar
· Kupitia
vifungu vinavyohusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuvitafakari upya
kwa minajiri ya kuimarisha zaidi muundo huo
3.3.
SHERIA ZINAZOHITAJI KUTAZAMWA UPYA
NA KUFANYIWA MABADILIKO
·
Sheria
ya Uchaguzi
·
Sheria
ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
·
Sheria
ya Gharama za Uchaguzi
·
Sheria
ya Usajili wa Vyama
4.1.
MUUNDO WA UTEKELEZAJI WA MABADILIKO
YA KATIBA NA SHERIA
Mabadiliko kama haya
yatahitaji uwazi na uwajibikaji ili yasilalamikiwe. Ili kuwezesha uwazi na
ushirikishi katika mchakato wa mabadiliko haya JUKATA tunapendekeza iundwe
kamati ya ufundi ya vyama vyote vilivyoko bungeni itakayoshirikiana pia na
ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya
Uchaguzi kuandaa miswada yote na kuipeleka bungeni katika bunge litakalokaa
Novemba 2014 kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza kabla ya wadau kutoa maoni
yao na kupitishwa rasmi mwezi Februari, 2015.
5.0.
HITIMISHO
JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA tunatoa tamko hili baada ya kufanya tathmini ya kina juu ya mchakato
wa Katiba Mpya ulipofikia kwa jicho la michakato mingine inayoendelea nchini.
Nia yetu ni kuhakikisha kuwa michakato hii inapata muda wa kutosha na kufanya
demokrasia ya ushiriki ipate nafasi katika michakato hii, hasa ule wa Katiba
Mpya. Itakuwa ni busara kwa vyombo na taasisi zilizopewa majukumu katika tamko
hili kupokea majukumu hayo kwa moyo mkunjufu na kuwa tayari kuyatekeleza bila
kuzidi kupoteza muda kwa mabishano mengine kama ilivyotokea mwanzoni mwa
mchakato unaoendelea wa Katiba Mpya nchini. Mabishano mengi ingawa yanaleta
afya kwa mchakato pia huwa na athari mbaya ya kuchelewesha utekelezaji wa hatua
husika. Itafaa sana kuweza kukubaliana mambo ya msingi yaliyopendekezwa na
kuanza utekelezaji kwa kuwa kwa muda uliobaki haiwezekani kutimiza ndoto zote
tulizonazo kwa ufanisi unaohitajika na bila kuleta madhara katika ubora wa
baadhi ya Michakato.
Kwa
umuhimu wa haja ya Mabadiliko ya Kikatiba na Kisheria kuhusu maeneo yenye
athari kwa uchaguzi, JUKATA tumeteua Jopo la Wanasheria na Wataalamu ili
kuandaa pendekezo la Masharti yote ya Katiba na Sheria yatakayoathiriwa na
mabadiliko hayo na kupendekeza jinsi yatakavyofanana katika sura zake Mpya
baada ya mabadiliko. Jopo hilo litaongozwa na Wakili Armando Swenya wa JUKWAA
LA KATIBA TANZANIA.
Imetolewa na
kutiwa Saini kwa niaba ya JUKATA na;
Deus M Kibamba
Mwenyekiti
25 Julai, 2014
No comments:
Post a Comment