Tamasha
la saba la Muziki wa Cigogo 2014, lililoanza jana Julai 25, kwenye
kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa linarindima kwa kishindo na
kufanya nji wote kuwa na shamrashara za aina yake.
Tamasha
hilo ambapo jana lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.
Rehema Nchimbi, linashirikisha vikundi zaidi ya 30 vikiwasha moto wa
ngoma na muziki wa kitamaduni.
Kwa
mwaka huu tamasha hilo ni la msimu wa Saba (7) likifahamika kama
(Wagogo music festival 2014) lenye kauli mbiu ‘Utamaduni na Amani’
linarindima kwa siku tatu na hiyo kesho Julai 27 linatarajia kufikia
tamati.
Mkurugenzi
mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana, wa Kituo cha Sanaa Chamwino
(Chamwino Arts Center-CAC) wandaaji wa tamasha hilo alisema wanatarajia
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, ndiye atakayelifunga rasmi tamasha hilo hiyo
kesho.
“Kesho Julai 27, ndiyo tunafikia tamati na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino anatarajia kuwa mgeni rasmi.” alisema Dk. Kedmon.
Tamasha
hilo tokea kuanza kwake limekuwa katika mwangaza mpana wa kukuza na
kuinua utamaduni wa Cigogo, ambapo kwa mwaka huu limeweza kukusanya
wasanii zaidi ya 700 na wageni mbalimbali katika mji huo wa Chamwino
Ikulu.
Aidha,
alivitaja vikundi vinavyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na kutoka
Dodoma kuwa ni New Pendo, Yelusalem, Inueni mioyo, Yeriko, Nyota njema,
Ushirikiano, Nyerere na Ebenezer.
Vikundi
vilivyo vijiji vya Wilaya ya Chamwino ni Upendo (Kijiji cha Dabalo),
Imani, Sinai (Kijiji cha Membe). Mchungaji mwema, (Kijiji cha Nzali),
Juhudi, Muhubiri (Kijiji cha Kawawa), Nyota njema, Safina, Ndagwa
(Kijiji cha Msanga).
Msifuni
(Kijiji cha Mlimwa), Nyota, Ufunuo (Kijiji cha Majeleko), Simba (Kijiji
cha Mbele zungu) na Inueni mioyo (Kijiji cha Mgunga).
Vikundi
kutoka Wilaya ya Kongwa imani ( Kijiji cha Mkutani), Faru (Kijiji cha
Songambele) na Safina (Kijiji cha Chigwingili), Pia kikundi cha Uvuke
na Upendo (kutoka Manispaa ya Dodoma mjini).
Vikundi
vingine ni Mandoo/Tasuba kutoka Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Nazareti (Dar
es s Salaam), Muungano (Manyoni, Singida) na Zanzibar.
SOURCE: FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment