Kambi Mbwana, Msemaji wa Taasisi ya Handeni Kwetu Foundation
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SIKU
chache baada ya kusajiliwa rasmi chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Taasisi inayojulikana kama Handeni Kwetu Foundation,
imepangwa kuzinduliwa August 5 mwaka huu, katika Ukumbi wa Vijana Social
Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Kuanzishwa
kwa taasisi hiyo ni kutafuta namna ya kusaidiana na serikali katika
mambo mbalimbali, ikiwamo Kujenga uwezo kwa jamii kujikwamua kiuchumi na
kuhamasisha utawala.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana,
alisema taasisi hiyo imeanzishwa na itafanya kazi zake bila kuvunja
masharti yaliyowekwa na serikali ili kuhakikisha kuwa malengo
yaliyokusudiwa yanapatikana.
Alisema
kuwa taratibu za kuelekea kwenye uzinduzi huo zinaendelea kuwekwa
katika hali ya kukutana pamoja kwa wageni walioalikwa kushuhudia
uzinduzi huo wa aina yake.
“Kwa
miezi kadhaa sasa taasisi ilikuwa kwenye mchakato wa usajili wake,
hivyo baada ya kukamilika, kinachofuata sasa ni kuzindua ili ianze kazi
zake kama ilivyokusudia.
“Taasisi
hii itakuwa na Makao yake Makuu wilayani Handeni, lakini itafanya kazi
zake nchi nzima na huko mbele itakuwa na ofisi katika kila eneo
itakaloona inafaa,” alisema.
Sababu
nyingine za kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuleta ustawi kwa jamii
katika njanya mbalimbali, kutoa mafunzo kuhusu kilimo bora na jinsi ya
kutafuta masoko, kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha misingi ya utawala
bora, kutoa elimu na ushauri kuhusu mbinu bora za kuimarisha afya na
elimu ya msingi kuhusu Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
Malengo
mengine ni kutoa elimu kuhusu makundi rika katika elimu ya uzazi,
kuhamasisha na kushawishi jamii kuzingatia ustawi wa mtoto katika jamii,
kufanya utetezi kwa makundi maalum ambayo haki zao zinakiukwa na
kufanya tafiti mbalimbali zenye malengo ya kuboresha maisha ya jamii,
kiuchumi na kijamii.
CHANZO: FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment