Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 27 July 2014

DAKTARI AFARIKI KWA EBOLA LIBERIA, ALIYETOROSHWA SIERRA LEONE AFARIKI PIA

Wauguzi wambeba mgonjwa wa ebola

Idara ya afya nchini Liberia imetangaza kuwa Daktari mmoja wa Ebola amefariki kutokana na viini vya ugonjwa huo.
Ni daktari wa kwanza nchini humo kufariki kutokana na ugonjwa huo tangu uzuke mapema mwaka huu.
Daktari Samuel Brisbane aliambukizwa viini vya ugonjwa huo alipokuwa akiwatibu wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.
Alihudumu kama daktari wa watu wengi maarufu akiwemo rais wa zamani Charles Taylor.
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa takriban watu 660 wamethibitishwa ama wanashukiwa kufariki na ugonjwa huo Magharibi mwa Afrika tangu mwezi February na kuufanya kuwa ugonjwa m'baya zaidi tangu uzuke.
Katika hatua nyingine, maafisa wa afya nchini Sierra leone wamethibitisha kwamba mgonjwa mmoja wa Ebola aliyetoroka hospitalini katika mji mkuu wa Freetown amefariki baada ya kurudi hospitalini.
Mwanamke huyo kwa jina Saudato Koroma ndio mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa huo mjini humo.
Alijiwasilisha hospitalini humo baada ya serikali kuwataka raia kupitia tangazo la redio kusaidia kumsaka.
Alifariki Wakati alipokuwa akisafirishwa na wazazi wake mashariki mwa Sierra Leone ambapo vituo vya kuwauguza wagonjwa wa Ebola vimejengwa.
Ugonjwa huo umewaua zaidi watu 660 Magharbi mwa Afrika mwaka huu.
BBC

No comments:

Post a Comment