Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki
Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya
kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar
es Salaam jana.
Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi
hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea
kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo
itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani.
Aidha,
Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali
nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo
inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa
mali za Kanisa.
Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema “Serikali
haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta
usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu ya Waumini wa
Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa
ajili ya kuliombea Taifa.
Maombi hayo yalifanyika katika Kituo cha
Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Chikawe ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini
kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka
kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia
katika uvunjifu amani makanisani.
Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro
katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika
kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi,
kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa.
Kutokana na migogoro
hiyo Chikawe alisema; “Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa
amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa
yenye migogoro ili kuepusha shari”.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment