Tanzania imekuwa moja ya nchi nne
Afrika iliyotunukiwa tuzo ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani na
Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga duniani (ICAO) kutokana na
mchango wake mkubwa katika ukuaji na usalama wa anga katika bara la
Afrika.
Tuzo hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Dakar, Senegal na
Rais wa ICAO, Dk. Bernard Aliu katika kikao cha 24 cha Kamisheni ya
usafiri wa anga afrika.
Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, John Chacha akipokea tuzo hiyo
kutoka kwa Rais wa ICAO, Dk. Aliu
CREDIT: FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment