THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@ googlemail.com
Website :www. ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania imepandishwa hadhi katika Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) na sasa inaweza kupata mikopo mikubwa zaidi na yenye hadhi
kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo katika
Tanzania, Bi. Tonia Kandiero ametangaza hayo, Julai 23, 2014.Bi.
Kandiero amesema kuwa miaka yote tokea Tanzania kuwa
mwanachama wa AfDB, imekuwa inapata mikopo ya hadhi ya chini zaidi na
midogo zaidi ya maendeleo kutokana na uwezo na nguvu za uchumi
wake.Amesema kuwa hadhi ya Tanzania ndani ya Benki hiyo imepanda
kutokana na kukua kwa uchumi wa Tanzania, kuongezeka kwa uwezo wa
kukopesheka na uwezo wa kulipa na kutimiza masharti yanayokwenda na
mabadiliko hayo ya hadhi.
Bi. Kandiero ametangaza mabadiliko hayo katika hadhi ya
Tanzania ndani ya Benki hiyo wakati alipozungumza katika sherehe kubwa
ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya
Mangaka-Mtambaswala kwa kiwango cha lami na kufungua Barabara ya
Masasi-Mangaka ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami. Barabara zote
ziko katika mkoa wa Mtwara na mgeni rasmi katika sherehe hiyo kubwa
iliyofanyika mjini Mangaka, mji mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, alikuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaJakaya Mrisho Kikwete,
ambaye ameingia Mkoani Mtwara jana kwa ziara ya siku mbili.
Ameingia Mtwara akitokea Ruvuma ambako alifanya ziara ya
siku sita.Bi. Kandiero amemwambia Rais Kikwete na mamia ya wananchi
waliohudhuria sherehe hiyo kuwa kabla ya kupandishwa hadhi, Tanzania
ilikuwa na sifa za kukopa ndani ya benki hiyo mikopo kutoka Mfuko wa
Maendeleo wa Benki hiyo na siyo mikopo mikubwa ya maendeleo.
Bi. Kandiero amesema kuwa tokea Tanzania kujiunga na AfDB
imepata kiasi cha mikopo ya thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni
moja.
AfDB ni moja ya wafadhili wa barabara hizo mbili ambazo
sherehe zake za uzinduzi na jiwe la msingi zimefanyika jana kwa
kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan
(JICA) na Serikali ya Tanzania.
AfDB na JICA zinashirikiana na Serikali ya Tanzania
kugharimia ujenzi wa barabara hizo chini ya Mradi wa kuendeleza Barabara
nchini. Chini ya ushirikiano huo, AfDB inatoa asilimia 64.79 kugarimia
ujenzi wa barabara hizo, JICA inatoa asilimia 31.83 na Serikali ya
Tanzania inatoa asilimia 2.39.Barabaraba ya Mangaka-Mtambaswala, mpakani
mwa Tanzania na Mozambique, ina urefu wa kilomita 65.5, inajengwa na
kampuni ya Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya shilingi bilioni
59.66 na ujenzi utakuchukua miezi 28.
Nayo Barabara ya Mangaka-Masasi yenye urefu wa kilomita 55.1 ilikamilika mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuwekewa jiwe la msingi la ujenzi wake na Rais Kikwete Agosti 21, 2009. Barabara hiyo, ilijengwa na kampuni kutoka Japan kwa awamu tatu na kwa gharama ya shilingi bilioni 54.8. Barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Masasi-Mangaka-Tunduru.
Nayo Barabara ya Mangaka-Masasi yenye urefu wa kilomita 55.1 ilikamilika mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuwekewa jiwe la msingi la ujenzi wake na Rais Kikwete Agosti 21, 2009. Barabara hiyo, ilijengwa na kampuni kutoka Japan kwa awamu tatu na kwa gharama ya shilingi bilioni 54.8. Barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Masasi-Mangaka-Tunduru.
No comments:
Post a Comment