Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 July 2014

RATIBA YA UCHAGUZI WA NDANI WA CHADEMA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RATIBA YA UCHAGUZI WA NDANI YA CHAMA
Ndugu wanahabari
Tunaomba kuanza press conference hii kwa kuendelea kuwashukuru kwa ushirikiano wenu mnaotupatia kila mnapokuwa mkitimiza wajibu na majukumu yenu kwa jamii.
Leo tunapenda kutoa kwa umma kupitia vyombo vya ratiba ya uchaguzi ya uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea nchi nzima kwa sasa, kama ilivyoazimiwa na Kamati Kuu iliyoketi Julai 18-20, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Itakumbukwa kuwa wakati tulipokutana nanyi hapa Julai 20, mwaka huu baada ya kikao hicho, tulisema kuwa kwa sababu Kamati Kuu iliazimia masuala mengi, itakuwa vyema tukiyawasilisha kwa wanachama na umma wa Watanzania hatua kwa hatua.
Katika kikao hicho, Kamati Kuu ilipokea taarifa ya sekretarieti, kujadili kuhusu zoezi la uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea nchi nzima, na kuazimia kama ifuatavyo;
1.2.1 Kamati Kuu iliazimia kuwa uchaguzi wa Baraza la wazee Taifa utafanyika mapema zaidi ili kuwawezesha kusimamia uchaguzi wa viongozi ngazi ya Taifa kwa mujibu wa katiba ya chama.
1.2.2 Kamati Kuu iliazimia kuwa uchaguzi ngazi ya Kanda utafanyika baada ya uchaguzi wa ngazi ya Taifa, ili kuwezesha Mkutano Mkuu kufanya maboresho ya Katiba kwa ajili ya kuwezesha ngazi hiyo kufanya uchaguzi kwa ufanisi zaidi
1.2.3 Kamati kuu imepitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ilivyopendekezwa na Sekretariati, kama ifuatavyo;
Hadi tarehe 30/07/2014- kukamilika uchaguzi wa kata
Hadi tarehe 15/08/2014- kukamilika chaguzi za majimbo/wilaya
Hadi tarehe 30/08/2014- kukamilika chaguzi za mikoa
Tarehe 6/09/2014- Uchaguzi wa Baraza la Wazee
Tarehe 10/09/2014- Uchaguzi BAVICHA
Tarehe 11/09/2014- Uchaguzi BAWACHA
Tarehe 12/09/2014- Kamati Kuu
Tarehe 13/09/2014- Baraza Kuu
Tarehe 14/09/2014- Mkutano Mkuu
Tarehe 15/09/2014- Baraza Kuu
Tarehe 16/09/2014- Kamati Kuu Mpya
1.2.4 Kamati kuu imeagiza kuundwa kwa kamati ya kusimamia uchaguzi wa ndani ya chama kwenye ngazi za Mikoa, Wilaya na Majimbo kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya
1.2.5 Kamati kuu inaagiza kuwa zoezi la kufanya ukaguzi wa uongozi ndani ya chama na utekelezaji wa Chadema ni Msingi ni endelevu.
1.2.6 Kamati Kuu imeiagiza Sekretariati kufanyia maboresho ya fomu za uchaguzi wa ndani ya chama na kuanza kuzisambaza kwenye ngazi husika kwa ajili ya kutumika katika uchaguzi Mkuu ujao wa ndani ya chama . Aidha Miiko ya Kikanuni kwa wagombea mbalimbali iwekwe kwenye fomu za kuomba kugombea uchaguzi kama sehemu ya fomu husika.

No comments:

Post a Comment