TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.07.2014
- MZEE WA MIAKA 75 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
- MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MZEE MMOJA MWENYE UMRI WA MIAKA 75
ALITAMBULIKA KWA JINA LA DAIMONI MATATA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUSINGO
ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA SHINGONI NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 02:00 HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUSINGO, KATA YA
SONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA.
AIDHA MTU MMOJA AMBAYE NI
MTOTO WA MAREHEMU AITWAYE WATSON DAIMONI (53) MKAZI WA KIJIJI CHA
LUSINGO AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – MBALIZI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
UPELELEZI ZAIDI JUU YA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITO KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
AIDHA
ANASHAURI FAMILIA ZIWE NA UTAMADUNI WA KUKAA NA KUTATUA KERO NA
CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO ZINAJITOKEZA KATIKA KAYA ZAO ILI KUEPUKA
MADHARA/MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BARAKA ZAWADI MJEMWA (31) MFANYABIASHARA NA
MKAZI WA MIKOROSHINI – KYELA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.604 BCS AINA YA TOYOTA NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE
ASAJILE AYUB (35) MKAZI WA KASUMULU KULIGONGA GARI JINGINE LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.649 ALB AINA YA TOYOTA HILUX LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE MUSA MWALUBANGE (32) MKAZI WA KIJIJI CHA MBUGANI NA KISHA
KUPOTEZA MWELEKEO NA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU HUYO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
29.07.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILAMBO,
KATA YA ITOPE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI NI BAADA YA GARI T.604 BCS KUTAKA KUYAPITA MAGARI
YALIOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA AMEKAMATWA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.
Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment