Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imekanusha tamko liliotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Elimu (THTU) na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) la kudai kwamba kuna
mpango wa kupunguza Mafao ya Pensheni ya wanachama mifuko ya LAPF na
PSPF.
Akizungumza
Dar es Salaam Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul
Kinemela alisema taarifa hizo sio za kweli ambazo kwa namna nyingine
zinalenga kupotosha umma.
”Tunaomba
wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umma kwa ujumla kuwa
kinachoendelea ni majadiliano na wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii
yenye lengo la kuboresha mafao ya wastaafu” alisema Kinemela.
Alisema
kuwa Chama cha Walimu Tanzania ( CWT) na THTU wakiwa ni wadau sekta ya
hifadhi ya jamii wanayo haki ya kikatiba ya kukutana na kujadiliana
masuala mbalimbali yakiwamo ya sekta ya hifadhi ya jamii.
Alisema Serikali inachukua fursa hiyo kuwatoa hofu wastaafu na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
”Tunaomba
wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa watulivu na kujiepusha na
maneno yoyote ya upotoshwaji na mwisho kuwachanganya wanachama na hivyo
kupunguza ufanisi wa kazi na utendaji,” alisema Kinemela.
IMECHOMOLEWA WANABIDII
No comments:
Post a Comment