TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza
la Madiwani la Manispaa yaa Kinondoni katika Kikao chake cha tarehe
22/07/2014 siku ya Jumanne, chini ya Mstahiki Meya Mh. Yusuph Mwenda
pamoja na mambo mengine lilijadili na kutolea maamuzi ya mashauri ya
mashtaka ya nidhamu yaliyofunguliwa kwa Watumishi 11 wa Idara mbalimbali
za Manispaa waliofanya makosa mbalimbali kama Utoro kazini, Matumizi
mabaya ya madaraka na ofisi.
Kati ya Watumishi 11 waliofunguliwa Mashtaka, watumishi 6 ni wa Idara ya Afya, 2 ni wa Idara ya
Elimu
ya Sekondari (Walimu wa Leseni) na 3 ni wa Idara ya Utawala na Utumishi
kada ya Maafisa watendaji wa Mitaa ambao ni 2 na polisi msaidizi 1.
Aidha
Baraza limefikia uamuzi wa kuwafukuza kazi watumishi 9 na kuwapa
karipio watumishi 2. Kati ya watumishi 9 waliofukuzwa kazi, watumishi 4
ni wa Idara ya Afya, 3 Idara ya Utawala na Utumishi ambao ni Maafisa
watendaji wa Mitaa 2 na Polisi Msaidizi 1, na 2 kutoka idara ya Elimu ya
Sekondari ambao ni walimu wa Lesseni.
Watumishi
2 waliopewa karipio kutoka Idara ya Afya wametakiwa kujirekebisha,
ambapo watakuwa katika uangalizi kwa muda kuona kama wamejirekebisha
mienendo yao.
Baraza la Madiwani limewataka
watumishi wote, kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na
maelekezo mbalimbali ya Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kutoa
huduma kwa Umma sambamba na kuheshimu maadili ya kazi zao kwa hekima na
busara, ili kuweza kutoa huduma bora kwa wakazi wa Kinondoni.
Aidha,
Baraza limesisitiza kuwa halitasita na litaendelea kuchukua hatua za
kinidhamu kwa watumishi wanao fanya makosa mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
SEBASTIAN MHOWERA
AFISA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.
No comments:
Post a Comment