Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni mia sita kutoa fedha hizo.
Limeonya kuwa vita vinavyoendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi huenda vikasababisha baa la njaa nchini humo.
Shirika la chakula duniani WFP limesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa watoto elfu hamsini huenda wakapoteza maisha yao kutokana na utapia mlo mwaka huu huku thuluthi moja ya raia wakikabiliwa na na viwango hatari vya njaa.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment