IGP Ernest Mangu
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Unapojibu tafadhali taja:
Anuani ya simu “mkuupolisi”
Simu : (022) 2110734
Fax
na. (022) 2135556
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.l.P. 9141,
Dar es Salaam.
26/07/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi
la Polisi Tanzania linapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote,
vyama vya siasa, taasisi mbalimbali za serikali, madhehebu ya dini,
asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa ushirikiano wa dhati katika
kusimamia masuala ya amani na usalama hapa nchini.
Tunapoelekea
kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi
linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo
kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu
wa amani.
Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani
ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu
pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya
starehe. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha
sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na
mikusanyiko hiyo ya watu.
Jeshi la Polisi
linapenda kuwaondoa hofu wananchi wote kuwa, limejipanga kikamilifu
kuhakikisha wananchi kote nchini wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na
utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za
bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote, aidha, tunapenda
kuwatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, kuwa
makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva
wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi
wawapo kazini.
Katika kuhakikisha usalama
kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na
matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa
kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita
kiasi.
Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru
wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya
starehe, hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu,
yakiwemo maduka, hoteli na maeneo ya benki. Aidha, Jeshi la Polisi
linaendelea kuwasisitiza wale ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka
ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji
endapo uhalifu unatokea.
Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio
mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.
Aidha
wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao wasiache nyumba
wazi ama bila mtu na watoe taarifa kwa majirani zao, na pale
wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe
taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao au kwa namba
ya simu ifuatayo 0754 785557, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa
haraka.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment