Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 July 2014

JACK WILSHERE AJUTIA UVUTAJI SIGARA


Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere amesema anajutia kitendo chake cha kupigwa picha akivuta sigara hadharani katika bwawa la kuogelea huko Las Vegas.
Wilshere mwenye miaka 22 amelaumiwa hasa kwa kuzingatia wakati picha hizo ziliposambaa timu yake ya Uingereza ilikuwa katika kipindi kigumu ikitolewa katika Kombe la Dunia hatua za mwanzo.
Hii ni mara ya pili Wilshere kufumwa akivuta sigara katika kipindi cha miezi tisa.
Mwezi wa kumi, Wilshere alipigwa picha akivuta sigara akiwa nje ya Klabu ya Usiku baada ya kuishinda Napoli.
"Ninajutia," alisema. "haikubaliki na nitakubaliana na matokeo kisha maisha yataendelea."
Meneja Arsenal, Arsene Wenger alimkosoa Wilshere na akasema ataongea nae kuhusu suala hili.

BBC

No comments:

Post a Comment