Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 26 July 2014

HADITHI YA MAPENZI YA CRISTIANO RONALDO NA IRINA SHAYK

21 Cristiano Ronaldo And Irina Shayk Love Story
Hadithi ya mapenzi baina ya Cristiano Ronaldo na mrembo Irina Shayk ilianza mwaka 2010. Tangu wakati huo uhusiano wao umepitia kwenye milima na mabonde, kuachana na kurudiana kupitia vyombo vya habari duniani (lakini siyo katika uhalisia) lakini pamoja na yote hayo Irina na Cristiano bado wako pamoja na kwa mujibu wa picha mbalimbali za wawili hao, wanaonekana wakifurahia maisha na uhusiano wao.
Wanapendeza sana - Irina ni mrembo mrefu wa Kirussia mwenye macho mazuri ya mvuto ambayo yanaelezwa ndiyo yaliyomroga Ronaldo akapagawa moyoni na nafsini mwake. Lakini mwanandinga huyo anayechezea klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno ni 'mtu wa watoto, umbile lake la kimichezo na sura jamali vimekuwa mvuto kwa wasichana wengi ulimwenguni kote huku utajiri wake ukiwa nyongeza nyingine inayomfanya apepee kwenye maraha. Lakini ukiwatazama wawili hao wanaonekana kubembea kwenye ulimwengu mwingine wa peke yao licha ya tetesi nyingi zinazowazunguka.
51 Cristiano Ronaldo And Irina Shayk Love Story
Ronaldo anatajwa kuwa ndiye mchezaji bora na ghali zaidi ulimwenguni, akiwa ameshinda michezo na mataji mengi na ni kijana anayevutia… hiyo haitoshi kumfanya msichana yeyote amzimikie ghafla? Inaonekana hapana – walau kama mwanadada huyu ni Irina Shayk, mmoja wa warembo wanaosifika zaidi duniani, na mwanamke mrembo zaidi ulimwenguni kwa mwaka 2013 kwa mujibu wa Maxim.
 Cristiano Ronaldo And Irina Shayk Love Story
Wakati walipokutana kwa mara ya kwanza, Cristiano, ambaye alikuwa na msululu wa wasichana warembo na mlolongo wa taarifa chafu na nzuri za mapenzi maishani mwake, akazama kwenye penzi ghafla. Alizowea kuwapagawisha wasichana wakamzimikia ghafla mara walipomuona, lakini safari hii hali ilikuwa tofauti. Irina ni msichana ambaye yuko makini mno kuweza kumzimia mwanamume ghafla.
61 Cristiano Ronaldo And Irina Shayk Love Story
Cristiano alikuwa na wakati mgumu kumfukuzia mpaka pale mwanadada huyo alipoamua mwenyewe kwenda naye kwenye safari ya mapumziko (holiday). Hivyo ndivyo uhusiano wao ulipoanza. Pamoja na maoni ya watu waliobashiri kwamba Ronaldo angemtosa mwanadada huyo haraka kama alivyofanya kwa wengine, hadithi yao ya mahaba imedumu kwa miaka minne sasa.
41 Cristiano Ronaldo And Irina Shayk Love Story
Irina hapendi kuzungumza hadharani kuhusu uhusiano wake na Ronaldo na kwa kawaida hujibu kwa misamiati ya kawaida inayowazuia watu wengine wasipekenyue maisha yake binafsi. Anaitahidi kukaa mbali na tetesi zote na anafurahia zaidi kucheza na mtoto wa Ronaldo pindi anapokuwa na muda. Lini watafunga ndoa? Ni swali ambalo linaweza kujibiwa na wao wenyewe.

No comments:

Post a Comment