Kukanusha taarifa
Katika
gazeti la Tanzania Daima toleo na.3536 la tarehe 30 Julai, kuna habari
inayosema Lowassa aibukia ACT na kumuhusisha na Mbunge wa Kigoma
Kaskazini(CHADEMA) Zitto Kabwe katika kile gazeti hilo kilichodai
mikakati ya siri dhidi ya Chadema.
Habari
hizo ni uzushi, na ni muendelezo wa mikakati ya kumchafua na
kumgonganisha Mh Lowassa na wanasiasa wenzake wa kada na maeneo
mbalimbali. Mh Lowassa kama walivyo wabunge wengine wa CCM amekuwa na
uhusiano na wabunge wenzake bila kujali tofauti ya vyama vyao.
Mh Lowassa ni kiongozi makini ambaye hawezi kupoteza muda wake kujiingiza katika masuala yasiyo na tija kwa nchi, wananchi na ustawi wa demokrasia makini na endelevu nchini. Muda wake anautumia kusimamia utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni kwake Monduli.
"Mimi na chama chetu, tuko busy kutekeleza ilani yetu,kuwaletea maendeleo wananchi ili wazidi kutupa ridhaa ya kuwaongoza katika chaguzi zijazo" alisema Mh Lowassa.

Hata
hivyo, Mh Lowassa anathamini mchango wa vyama vyote vya siasa nchini
pamoja na Chadema katika kujenga demokrasia yenye tija kwa taifa.
Imetolewa na ofisi ya Mh Edward Ngoyai Lowassa(mb)
No comments:
Post a Comment