Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 July 2014

HAYA NDIYO MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA STEVEN WASSIRA UBUNGO PLAZA


MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA
STEVEN WASSIRA UBUNGO PLAZA HAYA HAPA

Swali la Kwanza;Kama unaukataa muundo wa muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa na wananchi kupitia Tume ya Jaji Warioba kwa uchache wa Takwimu, wewe unapendekeza uwepo wa Serikali mbili kwa Takwimu zipi?.
Swali la Pili;Je, gharama za kuuendesha muungano huu wa Serikali mbili za sasa ni Shilingi ngapi, wananchi wa pande zote mbili tunataka ufafanuzi wa Serikali maana ni haki yetu ya kikatiba kufahamishwa gharama tunazotumia katika kuiendeshea Serikali yetu kama walipa kodi, ili tufahamu na tulinganishe na gharama zilizoainishwa na Tume ya Jaji Warioba kwenye muundo wa Serikali mbili kwa lengo la kupata ukweli wa hoja hii ya gharama.
Swali la Tatu;Awadhi alimuuliza Wassira kwamba, kama mgao wa mapato ndio kikwazo cha muundo wa Serikali tatu kwamba Zanzibar watadai 50% ya mapato ya muungano kama CCM wanavyotoa hoja, Kwani ni lini Zanzibar ilipewa 50% ya mapato yote?
Mbona miaka yote Zanzibar inapewa 4% (asilimia nne) ya mapato yote ya muungano?.
Swali la Nne;Kama muungano huu ni wa Nchi moja yenye Serikali mbili, ni kwa nini Rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na ni kwa nini apigiwe mizinga ishirini na moja kama Rais wa muungano?
Na kama hayo ni ya kweli, ni kwa nini hamtaki kukubali kwamba Tanganyika ndiyo iliyovaa koti la muungano baada ya Zanzibar kutambuliwa na Katiba yao kama Nchi yenye mamlaka kamili?
Pia ni kwa nini mnakuwa ving'ang'anizi hata kwenye hoja za kweli na zenye ushahidi wa wazi hata inafikia hatua hamtaki kukubali kwamba muungano huu ni wa Nchi mbili zenye Serikali mbili badala ya muungano wa Nchi moja yenye Serikali mbili?
Hapa hakuna muungano bali hiki ni kiini macho, tunaitaka Tanganyika yetu sasa, na wazanzibar wanaitaka Zanzibar yao huru, maana nusu karne ya unafiki na uongo wa CCM umefika mwisho sasa.
Swali la Tano;Kama mnaukataa muundo wa Serikali tatu, ni kwa nini Katiba hii iliyopo hivi sasa ya mwaka 1977 inatambua uwepo wa muundo huo wa Serikali tatu na hata kufikia hatua ya kuwataja mawaziri watatu kwa kila Wizara, ikiwa na maana kwamba, Waziri anayeshughulikia mambo ya muungano kwenye Wizara husika ndani ya Bunge la muungano, Waziri wa Wizara husika na Waziri anayehudumu kwenye Bunge la wawakilishi Zanzibar?
Swali la Sita;Tume zote zilizowahi kuundwa ili kukusanya maoni ya wananchi tangu uhuru mpaka leo, nikiwa na maana ya Tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Jaji Nyalali, kundi la G55 na hii ya sasa chini ya Jaji Warioba, zote zimeleta maoni na mapendekezo ya wananchi yenye muundo wa Serikali tatu.
Licha ya kwamba michakato yote hii ya Katiba mpya tangu enzi hizo mpaka leo imekuwa ikiwagharimu walipa kodi wa Taifa hili mabillioni ya Shilingi, ni kwa nini kwa miaka yote hiyo mpaka leo Serikali hii ya CCM mmekuwa mkiikwepa hoja hii ya msingi inayopaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya Taifa zima.
Lakini pia, mbona tunazo timu tatu za Taifa za mpira wa miguu?
Kwani Zanzibar Hilloes ni ya wapi kama sio ya Zanzibar?
Kwani Kilimanjaro Stars ni ya wapi kama sio ya Tanganyika?
Kwani Taifa Stars ni ya wapi kama sio Timu ya muungano?
Kuna hoja gani nyuma ya pazia, inayowafanya muendelee kuifanya Zanzibar kama koloni la Tanganyika?
Nusu karne ya uongo ubabe na unafiki wa CCM na vibaraka wao, imefika mwisho sasa kwa sababu hiki sio kizazi cha analogia tena bali ni kizazi cha digital.
Tunautaka ukweli na uwazi katika masuala nyeti na ya msingi kama hili la kuivua Tanganyika Joho la muungano.
Mwisho!
Imeandaliwa na;
Francis Boniface Garatwa,
Mwanaharakati wa CHADEMA,
Kanda ya Ziwa Mashariki,
Mkoa wa Mara,
Wilaya ya Serengeti.
28/07/2014.
Email:francisboniface50@gmail.com
0785881009/0767881009.
*********************
Naomba kuwasilisha!
Ahsanteni sana!!!

Credit Source: Wanabidii

No comments:

Post a Comment