Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.
Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari Dar es Salaam leoasubuhi, wakati akitoa taarifa ya kituo hicho
ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi kufikia Juni 2014. Kulia
ni Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na
Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo. Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
KITUO cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuwa hadi kufikia Juni 2014
wanawake na wasichana 2,878 wamebakwa nchini kutokana na vitendo vya
ukatili dhidi yao.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen
Kijo-Bisimba wakati akitoa taarifa ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia
Januari na Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo.
“Vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya makundi hayo vilivyoripotiwa polisi kwa nchi nzima vilikuwa 3,633″ alisema Kijo -Bisimba.
Kijo-Bisimba
alisema taarifa hii inatoka na tafiti zilizofanywa na kituo hicho ili
kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa waangalizi wa haki
za binadamu, wasaidizi wa sheria, taarifa rasmi kutoka taasisi za
Serikali, Bunge, Mahakama,vyombo vya habari na asasi mbalimbali zisizo
za kiserikali.
Akizungumzia
kuhusu taarifa ya Sensa ya watu na makazi inaonesha idadi kubwa ya watu
wanaishi vijijini huku wakiwa na huduma duni za kijamii kama za afya,
maji, umeme, umeme na shule.
Alisema
takwimu zinaonesha bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana
na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi, mfano katika suala la
upatikanaji maji makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo
salama ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi
nzima.
Kuhusu
kilimo alisema idfadi ya wananchi wengi wapatao 11,359,090 wanategemea
kilimo kama shughuli kuu ya uchumi hata hivyo wakulima wengi bado
wanatumia jembe la mkono.
“Uwekezaji
katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa mfano mashamba
makubwa ya mpunga yaliyokuwa ya Shirika la NAFCO wilayani Mbarali mkoani
Mbeya wamepewa wawekezaji na wakulima wazawa wametengewa yasiyofaa”
alisema Kijo-Bisimba.
Credit Source: Fullshangwe
No comments:
Post a Comment