Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 26 July 2014

MWIGULU NCHEMBA ATEMA CHECHE MWANZA


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot
MWANZA: Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, amesema serikali imetoa msisitizo wa kupiga marufuku ununuzi wa mashangingi na matumizi mabaya ye fedha huku akihoji uhalali wa maofisa wa kawaida kutumia magari hayo gharama hata wanaoishi Masaki.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jioni hii, Nchemba amesema ni marufuku kwa wizara na idara za serikali kununua mashangingi huku akibainisha kwamba serikali imepunguza kwa asilimia 50 ununuzi wa magari hayo na kwamba utaratibu wa sasa utakuwa kununua magari ya mkupuo na kupewa watu maalum.
"Tumesema na tunasema ni marufuku kununua magari haya makubwa... gari linanunuliwa kwa shilingi milioni 200 na linatumiwa na ofisa wa kawaida anayeishi pale Mikocheni, haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zingetosha kabisa kujengea zahanati," alisema.
Ameongeza kusema kwamba, idara zote za umma zinatakiwa kubana matumizi badala ya maofisa kujipangia posho kubwa kubwa kwa matukio ambayo hayamnufaishi mwananchi wa kawaida, huku akitolea mfano maadhimisho ya siku mbalimbali ambayo hutengewa mamilioni ya fedha zinazoishia kwa maofisa kujilipa posho.
"Kila mwaka kuna maadhimisho, mara Siku ya Ukimwi... Siku ya Dawa za Kulevya.... Siku ya Mtoto wa Afrika... ni nyingi mno zaidi ya 60, ambapo mwaka mzima watu wanashughulika na maadhimisho haya na kuteketeza fedha kwenye kamati huku wakijaza mifuko yao... nimesema utaratibu unaandaliwa ambapo matumizi yanatakiwa yapungue," alisema.
Hata hivyo, ameitaka serikali kukusanya kodi kwa bidii ili kuondokana na utegemezi kwani hata deni la taifa lililopo linatokana na mapato ya serikali kuwa kiduchu.
Amesema ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma umetegemea zaidi mikopo kutoka mifuko ya ndani ya akiba za wafanyakazi, lakini kama kodi zingekusanywa kwa bidii, chuo hicho kingejengwa kwa fedha za serikali na siyo mkopo.
Ameongeza kwamba, ni lazima wafanyabiashara wakubwa walipe kodi ili wananchi wa kawaida waweze kunufaika na pia kupunguza pengo la umaskini miongoni mwa wananchi.
Kuhusu suala la Katiba Mpya, Nchemba amesema ni suala nyeti lakini anashangazwa na jinsi watu wanavyolichukulia kimzaha mzaha huku akisema wengi wanaangalia maslahi yao binafsi badala ya taifa.
"Watu wanalichukulia suala la Katiba Mpya kimzaha mzaha tu, wengine wanasema eti osho haitoshi... nasema hivi, anayedhani posho haitoshi aondoke," alisema.

No comments:

Post a Comment