Serikali ya Libya imeomba msaada wa kimataifa ilikuzima moto mkubwa unaoendelea kuchoma hifadhi ya mafuta mjini Tripoli baada ya makombora ya wapiganaji wa Kiislamu kulipua hifadhi ya takriban lita milioni 6 ya mafuta yaliyosafishwa.
Serikali hiyo changa inayoyumbishwa na mapigano baina ya makundi yanayopinga utawala uliomrithi Kiongozi wa miaka mingi Maummar Gaddaffi aliyeuawa katika mapinduzi ya 2011.
Msemaji wa kampuni hiyo Mohamed Al- Hariri anasema kuwa ikiwa moto huo utasambaa hadi kwenye mapipa mengine yaliyoko karibu basi itakuwa ni janga.Pipa hilo ni moja ya maghala yanayomilikiwa na kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini Libya - Brega
Serikli ya mpito nchini Libya imetaka kusitishwa mapigano ili kuruhusu wazima moto kuendelea na shughuli zao.
Takriban watu 97 wamekufa kufuatia mapigano baina ya makundi hayo hasimu ya waasi wanaotaka kumiliki uwanja wa kimataifa wa ndege wa Tripoli.
Katika mji wa Benghazi mapigano yamechacha na kusababisha vifo vya watu 38 siku ya jumapili.
Mataifa kadhaa yameelezea niya yoa ya kutuma msaada wa kuzima moto huo lakini wanazongwa na tahadhari iliyotolewa na mataifa ya Magharibi yaliyopelkea kuondoshwa mara moja kwa Wafanyi kazi wao na raiya wao nchini Libya wakiongozwa na Marekani iliyofunga Ubalazi wake.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli Rana Jawad amesema kuwa wakaazi wa Tripoli wametahadharishwa kuhama makwao kabla makao yao hayajaghubikwa na moto unaotarajiwa kusambaa iwapo hautadhibitiwa haraka.
Ufaransa ilifuta mkondo wa Marekani ilipoagiza raiya wake wote waondoke nchini humo.
Mwito sawia na huo ulitolewa na Ujerumani Uingereza na Uturuki na Umoja wa Mataifa UN.
Wakati huohuo Serikali ya Libya imeziomba makundi yanayopigana kusitisha mapigano ilikuruhusua wazima moto kuingia katika eneo hilo la uwanja wa ndege na kusadidia kuuzima moto huo unaozidi kuwa mkubwa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Libya Revolutionaries Operations Room (LROR) wanakabilianana kundi la Zintan likitaka kuingoa Zintan kutoka eneo hilo.
Mapigano haya ndiyo mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuondoka kwa Col Gaddafi.
Huko Benghazi, kundi la wapiganaji wanomuunga mkono generali aliyeaasi Khalifa Haftar linaendelea kukabiliana na majeshi ya Serikali.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment