Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Serekali
imeagiza bonde la mto Pangani na Halmashauri ya Jiji la Arusha
inapopima maeneo kuhakikisha inawashirikisha wananchi ili kuondoa
migogoro inayojitokeza ya kugmbea maji na kusababisha madhara makubwa
ikiwemo uvunjifu wa amani.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
anayeshughulikia Mazingira, Dk. Binilith Mahenge, alipokuwa
akihitimisha ziara yake baada ya kutembelea chanzo cha maji
kinachomilikiwa na Shamba la Kahawa la Burka Coffee Estate Limited jijini Arusha.
Alisema Bonde la Mto Pangani na Halmashauri ya Jiji ni lazima kushirikiana
wakati wa kupima maeneo yote ambayo ni vyanzo vya maji kwa kushirikisha
wananchi ili kuondoa migogoro ya kugombea maji inayojitokeza mara kwa
mara na kusababisha uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali.
Waziri
alisema mara baada ya kupima ni lazima vijengewe na kulindwa ili
wachache wasije wakageuza matumizi na kusababisha walio wengi kukosa
maji ambayo ni haki ya kila mmoja na pia maji ni uhai wa viumbe.hivyo
chanzo hicho ni muhimu kitunzwe na kuboreshwa kwa kuwa kinatumiwa na
wananchi wengi wakazi waliopo jirani katika maeneoya Burka na Olasti
Alisema
katika baadhi ya maeneo nchini kumekuwepo na migogoro kati ya wananchi
na wawekezaji kugombea vyanzo vya maji hivyo umefika wakati maeneo yote
ya vyanzo vya maji yakapimwa na kuwekewa taratibu na hivyo kuondoa
migogoro inayojitokeza.
Kwa
upande wake mkuu wa Bonde la Mto Pangani, Joel Lao, alisema inakadriwa
miaka kumi ijayo maji katika chanzo hicho yatapungua kutokana na
ongezeko la watu, hivyo kuna haja ya kutafutwa chanzo kingine .
Alisema
chanzo hicho kimeweza kutunzwa na kuwa cha kuvutia kwa mazingira
kutokana na kuwa ndani ya Shamba ambalo linaendelkezwa na kulindwa hivyo
kuzuia wavamizi wasiweze kuingia na kuendesha shughuli zisizo rasmi
ambazo haziendani na uhifadhi wa mazingira.
Awali
meneja wa shamba hilo Hamza Kassim, alisema kuwa shamba hilo lilimilikishwa chanzo hicho mwaka 2006 na Bonde la Mto Pangani na
kuwekewa, mifereji ya maji kwa ajili ya umwagiliaji, waliwekewa mita ya
maji ili kuelewa kiwango cha matumizi ambayo hulipia huku wananchi
wakitumia maji hayo bila mita hivyo haifahamiki kiwango cha maji
wanachotumia.
Alisema
kuwa Shamba hilo limeendelea kukitunza chanzo hicho, na mwaka jana
wananchi zaidi ya 400 waishio maeneo ya jirani ya chanzo hicho, ya
Olasti na Burka, walivamia chanzo hicho kusababisha uharibifu mkubwa
kwa kisingizio cha kukosa maji.
Meneja
huyo alisema maji yalipungua kutokana na ukame uliojitokeza kwa kipindi
kirefu na hivyo wananchi walidhania kuwa wamenyimwa maji na shamba hilo
na hivyo kuamua kujikusanya na kuvamia na kufanya uhalibifu mkubwa wa
mali.
Alisema
shamba hilo linatumia chanzo hicho cha maji kwa shughuli za umwagiliaji
wa kilimo cha Kahawa na maji mengine huwa yanaelekezwa kwa wananchi na
kunapotokea ukame maji hupungua jambo ambalo wananchi hudhania
wananyimwa maji.
Meneja
alisema kuwa wamekuwa wakifanya mikutano mingi na wananchgi ili
kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo wa maji lakini hadi leo hakujapatikana
muafaka.
Kutokana
na hali hiyo wanaomba msaada ili kuweza kupatikana kwa muafaka kati ya
shamba hilo la mwekezaji na uongozi wa serikali za maeneo hayo .
Source Credit: Fullshangwe
No comments:
Post a Comment