Shirika la kutetea Haki za Binadamu duniani, Amnesty International limesema chama kinachotawala nchini Burundi kimekuwa kikiendesha harakati za vitisho dhidi ya wale wanaonekana kwenda kinyume na serikali.
Katika ripoti mpya Amnesty limesema Umoja wa vijana wa Chama hicho unaojulikana Imbonerakure kimekuwa kikiwadhalilisha, kuwashambulia na kuwaua wafuasi wa upinzani.
Ripoti imesema makundi ya upinzani yamekuwa yakizuiwa kufanya mikutano ya hadhara na kufanya maandamano.
Inaaminika kuwa Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ana mpango wa kugombea urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka kesho.
BBC
No comments:
Post a Comment