Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dk. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia
damu katika zoezi lilioendeshwa na Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) katika kuchangia
damu mkoani humo. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali
Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine, uhaba unaofikia nusu kwa nusu ikilinganishwaan kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. Uhaba huo
umesababishwa na mwamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na
hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji huo una madhara. Madaktari wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na
watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa
wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo na kujitokeza kuchangia
damu kuokoa maisha ya Watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wakichangia damu.
Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dk. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
Dk. Marwa akichangia damu.
Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)
No comments:
Post a Comment