Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 July 2014

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI, NA WA UJERUMAN NCHINI TANZANIA NA KUMKARIBISHA MPYA WA UJERUMAN

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi, Luteni Jenerali Wyjones Matthew Kisamba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kumuaga akielekea kuanza kazi. Picha na OMR
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi, Luteni Jenerali Wyjones Matthew Kisamba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kujitambulisha kuanza kazi. Kushoto ni aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake. Hans Koeppel. Picha na OMR
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na  Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kujitambulisha kuanza kazi.
03
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake, Hans Koeppel  wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake. Kushoto ni Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke, aliyefika kujitambulisha kuanza kazi. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment