Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 30 July 2014

AJALI MBAYA ASUBUHI HII: BASI LA MOROBEST LAUA 15 PANDAMBILI



Picha kwa hisani ya JamiiForums

Na Japhet Malongo, Brotherdanny5.blogspot

PANDAMBILI, DODOMA: Takriban watu 15 wamekufa papo hapo na wengine 40 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Morobest kutoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori la masafa marefu katika Kijiji cha Pandambili wilayani Kongwa, takriban kilometa 100 kutoka Dodoma mjini.
Waliokufa papo hapo ni pamoja na madereva na makondakta wa basi pamoja na lori hilo ambapo ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:00 asubuhi hii.
Mashuhuda wa wanasema ajali hiyo imetokea wakati dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T820CKU kutaka kulipita gari jingine na ndipo lilipokutana uso kwa uso na basi hilo lenye namba za usajili T258ARV.
Inaelezwa kwamba, lori hilo lilikuwa limebeba mabomba makubwa likisafirisha kwenda nje ya nchi na baada ya kugongana mabomba hayo yakafyatuka na kuliponda basi, hali iliyosababisha vifo vya abiria wengine.
Hata hivyo, mpaka sasa idadi ya waliokufa imeongezeka na kufikia 20.
Tutaendelea kuwaleta taarifa zaidi kutoka eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment