Na Mahmoud Ahmad, Arusha
JUMUIA
ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi, taifa, imeahidi kupeleka timu ya
wakaguzi ili kubaini watumishi ambao wamejinufaisha na fedha za
uendeshaji wa shule ya sekondari ,Leguruki iliyopo halmashauri ya wilaya
ya Meru, inayokabiliwa na madeni mengi.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa Arusha, Daniel
Mgaya, kwenye hafla ya uzinduzi wa mtambo wa umeme unaotumia nishati ya
jua,Solar kwenye shule hiyo, amesema kuwa makao makuu ya jumuia ya
wazazi itatuma wakaguzi hao haraka mara baada ya sherehe ya sikuku ya
Idd el Ftri.
Alisema
kabla ya ufisadi uliofanywa na baadhi ya watumishi hao shule hiyo
ilikua na uwezo wa kujiendsha pasipo kutegemea mchango wowote toka nje
na kwamba hawatakuwa tayari kuona shule hiyo ikiadhirika huku
ikijulikana wazi watu walioifikisha shule hiyo mahali hapo.
Pia
aliwatoa wasiwasi watumishi wa shule hiyo pamoja na wazazi juu ya uvumi
kuwa shule imeshindwa kujiendesha na kwamba ipo katika hatua za mwisho
za kufungwa na kwamba jumuiya yake haiko tayari kuifunga shule hiyo
hivyo wazazi na watumishi waendelee kuiamini shule hiyo.
“Wazazi
pamoja na walimu wangu msiwe na wasiwasi shule hii haifungwi endeleeni
kuchapa kazi na leteni watoto wenu shuleni ila ninachowaahidi baada ta
ya sikukuu hii tutatuma timu ya wakaguzi kukagua mahesabu haiwezekani
watu waibe fedha halafu wapite mitaani kutangaza shule imekufa na
inafungwa”alisema Mgaya.
Aidha
mkuu wa skull hiyo Emanuel Loyi alisema kuwa skulli hiyo imekuwa
ikishindwa kujiendesha kutokana na deni kubwa la zaidi ya tsh million 24
hivyo ufungaji wa nishati hiyo uliofanywa na wafadhili kutoka nchini
ubelgiji kutoka shirka la Energy Assintance na kugharimu kiasi cha tsh
million 55 hivyo itaongeza kiwango cha ufaulu .
Alisema
madeni hayo ameyarithi kutoka kwa uongozi uliopita tangu mwaka
1991ambayo ni yale ya makato ya NSSF yaliyosababisha kufungiwa
kabisa.Mzabuni wa chakula cha shule pamoja na mishahara ya walimu hali
ambayo inashusha ari ya walimu kufanya kazi kwa bidii.
Kufuatia
hali hiyo Loyi aliuomba uongozi wa jumuiya hiyo kupitia kwa mgeni rasmi
ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Arusha Bernard Murunya kwa
niaba ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa Abdalah Bulembo kuandaa
harambee ya kukusanya fedha kwaajili ya kulipa madeni hayo na mambo
mengine ikiwemo kukamilisha ujenzi wa mabweni.
Naye
katibu wa wakuu wa skulli za sekondari mkoa wa Arusha Upendo Kakana
aliiomba serikali ya Chama Cha Mapinduzi kusimamia sera yake ya uwekaji
wa maabara katika kila shule za sekondari nchini ili kuweza kuinua zaidi
kiwango cha elimu.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoani hapa Bernad Murunya
aliahidi kufanyika kwa haraka kwa harambee hiyo iliyoahirishwa mwaka
jana ili kuiondoa shule katika tatizo hilo la madeni sugu pamoja na
kuboresha miundo mbinu yake ikiwemo umaliziaji wa mabweni.
Aidha
aliahidi kuboreshwa kwa miundo mbinu ya shule hiyo ili kuongeza kiwango
cha wanafunzi ambapo tayari katika suala la taa limeshapatiwa ufumbuzi
kupitia msaada huo na kilichobaki na ujenzi wa darasa la kompyuta
kwaajili ya walimu kufundishwa ili nao wawafundishe wanafunzi wao.
Watumishi wanaodaiwa kuondoka shuleni hapo ni pamoja na aliyekuwa mhasibu,mwalimu mkuu aliyegombea udiwani na walimu wengine.
CREDIT: FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment