Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 1 July 2014

UKOSEFU WA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WACHUNGAJI CHANZO CHA INJILI KUYUMBA, WAUMINI WAAMKA WACHANGA MILIONI 3 KWA AJILI YA UNUNUZI WA GARI


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

ARUSHA: IMEELEZWA kuwa kutokana na ukosefu wa vyombo vy ausafiri kwa wachungaji na viongozi mbalimbali wa makanisa wakati mwingine ndio chanzo kikubwa sana cha injili kutofika sehemu inapohitajika.
Pia ukosefu huo wakati mwingine husababisha hata huduma za kanisa kushindwa kutimia kwa wakati hali ambayo kwa sasa waumini wanatakiwa kuangalia vyombo muhimu ambavyo wachungaji wao wanatakiwa kuwa navyo ikiwemo suala zima la usafiri.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Nkirwa Palangyo kutoka katika Kanisa la Pentekoste imani na matendo lilopo maeneo ya kisongo jijini Arusha wakati waumini hao wakifanya harambee maalumu ya kununua gari la mchungaji wao mapema wiki iliyopita.
Mchungaji Palangyo aliongeza kuwa chombo kama gari kina umuhimu mkubwa sana kwenye maendeleo ya kanisa lolote lile kwani linaweza kurahisisha kazi mbalimbali za huduma hivyo basi ni changamoto kubwa sana kwa waumini kuhakikisha kuwa wanaliangalia suala hilo kwa undani sana. 
Alisisitiza kuwa wakati mwingine Injili inashindwa kufikiwa kwa wakati maalumu tena hasa maeneo ya vijijini kwa kuwa hakuna usafiri wa kufika huko ila kama kukiwa na magari ya kufika huko ni raisi sana wengi kuweza kumpokea bwana Yesu.
"Kanisa kama kanisa likiwa na usafiri wake basi linaweza kueneza injili kwa haraka sana tofauti na sasa ambapo wakati mwingine tunatamani kufika mbali ila tunashindwa kwa kuwa hatuna usafiri ni vema kama waumini wenyewe sasa hata wa makanisa mengine wakajifunza hili na kisha wakaanza utaratibu wa kutafuta magari ya watumishi wao," aliongeza Mchungaji Palangyo.
Awali mgeni rasmi katika harambee hiyo ambayo iliwashirikisha Wakristo kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha Isaya Sizya alisema kuwa Wakristo wengi wanashindwa kubarikiwa kwa kuwa wana mikono mifupi mbele za Bwana (wachoyo) na hivyo kila mara wanajikuta wakiwa wanabaki
maskini.
Sizya alidai kuwa wapo baadhi ya wakristo ambao kwa sasa wapo radhi waweze kuwekeza katika mambo ya dunia zaidi kama ili waweze kuonekana kwa ufarahari lakini kwenye michango ya makanisa wanakaa nyuma sana jambo ambalo sio sawa mbele za Mungu.
"tunatakiwa kujifunza kumtolea bwana sisi wakristo na tuhakikishe kuwa kwenyemichango ya makanisa tunakuwa mstari wa mbele tusibaki nyuma na kisha kuona mambo ya dunia ndio muhimu kwa kweli tutakuwa tunajiharibu sisi wenyewe ni lazima tubadilike sana kwenye hili na tuangalie mahitaji muhimu ya wachungaji wetu;aliongeza Sizya.
Katika harambee hiyo kiasi cha zaidi ya Milioni tatu kiliweza kupatikana kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ununuzi wa gari la mchungaji wa kanisa hilo la Pentekoste imani na Matendo.

No comments:

Post a Comment