Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 24 July 2014

ISRAEL YASHAMBULIA SHULE YA UN GAZA, 15 WAUAWA 200 MAJERUHI

Israili imeshambulia makao ya wakimbizi kati shule ya Umoja wa Mataifa huko Gaza .
Takriban watu 15 wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa vibaya baada ya majeshi ya Israeli kulipua shule inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa kuwahifadhi wakimbizi wa ndani kwa ndani wanaotoroka mashambulizi ya Isareli katika ukanda wa Gaza .
Wizara ya Afya katika ukanda wa Gaza imedhibitisha shambulizi hilo katika shule hiyo iliyoko Beit Hanoun ambayo inatumiwa kama makazi ya wakambizi wapalestina wanaotoroka makombora ya Israili.
Shambulizi hilo ni la nne kutokea katika vituo vinavyomilikiwa na Umoja wa Mataifa tangu Israeli ivamie ukanda huo yapata majuma mawili yaliyopita.
Kufikia sasa Wapalestina 725 wameuawa .
Waisraeli 30 wameuawa wengi wao wakiwa ni wanajeshi katika siku 16 za makabiliano kati ya Israeli na Hamas.
Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
Awali mwsimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia maswala ya Misaada bi Valerie Amos alisema kuwa hali ya maisha imeendelea kuzorota katika ukanda huo na kuwa kuna haja ya dharura ya kusitishwa kwa vita ilikufanikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu .
Bi Amos alisema kuwa watu laki moja (118,000) wanaishi katika kambi za umoja wa mataifa zilizoanzishwa katika shule zinazoendeshwa na UN.
Mkuu huyo wa UN alisema kuwa maji yamepungua na chakula pia hakitoshi kuwalisha wakimbizi hao wote .
Bi Amos amesema kuwa asilimia 44% ya Gaza hapakaliki kwa Wapalestina.

Hayo yamejiri baada ya Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa anasikitikia vifo vya Wapalestina lakini wajibu unamtegemea kiongozi wa Hamas ambaye bado anashikilia kuwa Israeli hainabudi kukoma kuikalia Gaza kimabavu.
BBC

No comments:

Post a Comment