Afisa wa shirika la umoja wa mataifa nchini Iraq ,Jacqueline Badcock ameonya kuwa agizo hilo la kidini ama Fatwa itawaathiri zaidi ya wanawake milioni nne kati ya umri wa miaka 11-46.
Kundi hilo linalosheheni wapiganaji wa dhehebu la Sunni ndilo linaloendeleza wimbi la mashambulizi katika taifa hilo linalotishia kusambaratika katika ya maeneo yanayotawaliwa na madhehebu.Kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu ndilo linaongoza mashambulizi katika maeneo ya Kaskazini mwa Iraq na wao ndio wanaotawala mji wa Mosul.
Ukeketaji sio kawaida nchini Iraq.
Mapema juma hili, Isisi iliwalazimisha Wakriso katika mji wa Mosul kuondoka na kuandika herufi N kwenye nyumba zao, hatua ambayo imetambuliwa kama kutaifisha mali za Wakristo katika eneo hilo.
Kulingana na amri hiyo mpya iliyotolewa chini ya Sharia, , wanawake wote kati ya umri wa miaka 11 na 46 wanapaswa kukeketwa.
Alisema hayo alipokuwa akiwahutubia waandishi wa habari kupitia simu ya video katika mji mkuu wa Mkoa wa Kurdi wa Ibril.
Zoezi hilo la kuwapasha tohara wanawake limeenea sana katika mataifa mengi ya Afrika mashariki ya kati na jamii kadhaa barani Asia.
Baraza la Umoja wa mataifa lilipitisha mswada mnamo mwaka wa 2012 ya kuharamisha tamaduni hiyo ya upashwaji tohara kwa wanawake.
Isis ilitwaa mji wa Mosul mnamo mwezi wa Juni miongoni mwa miji mingine midogo midogo kuelekea mji mkuu wa Baghdad.
BBC
No comments:
Post a Comment