Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
IMEELEZWA kuwa ili wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini waweze kupenda shule na kuthamini masomo walimu wanatakiwa kuwa na lugha pamoja na malezi yenye upendo wa hali ya juu tofauti na sasa ambapo zipo baadhi ya shule ambazo zina walimu wasiokuwa na upendo.
Aidha kwa sasa wanafunzi wengi watoro wanakwepa shule kwa kuwa wamekosa matumaini ya upendo toka kwa walimu wao hivyo basi walimu wanapaswa kubadilika.
"Tujifunze kwenye hizi shule ambazo zinaongoza kitaifa jinsi ambavyo walimu, bodi za shule zinavyowapenda wanafunzi,kwa hali hiyo basi mimi nasisiiza kuwa ili elimu iweze kufika katika kiwango cha juu lazima kwanza walimu wawe na upendo na wanafunzi ambao wanawafundisha," aliongeza Kanali Mongi.
No comments:
Post a Comment